Header Ads

MAMA STEVE AANIKA SABABU ZILIZO MFANYA AMUACHE BARNABA ||

Mzazi mwenzake na msanii Barnaba, Zuunamela maarufu Mama Steve, amefunguka kuwa moja ya sababu ya yeye kuachana na mzazi mwenzake ni usaliti ambapo Barnaba alipata mtoto mwingine wakati wakiwa pamoja.

Mama Steve amefunguka hayo mbele ya camera ya eNEWZ katika uzinduzi wa Album ya Barnaba inayoitwa Gold, ambapo yeye ni moja ya watu walioshiriki katika uzinduzi huo.

Alipioulizwa kuhusu mtoto wa kike ambaye amekuwa akionekana na Barnaba endapo alipatikana wakiwa wameachana au wako pamoja, alifunguka haya, "Yule mtoto amepatikana wakati mimi nikiwa naye pasipo mimi kujua kwa hiyo siwezi kuliongelea sana ila yeye mpaka aliamua kwenda kuvua bila kutumia kinga huenda alijiandaa au alidhamiria au ilikuwwa bahati mbaya au alikuwa ni mtu ambaye alikuwa nae muda mrefu kwa hiyo kwa hilo siwezi kuliongelea sana". Mama Steve aliendela kupigilia msumari kwa kusema kitendo cha Barnaba kwenda kumpa mwanamke mwingine mimba wakati anajua yuko na yeye alikichukulia kama dharau na  hiyo ni moja kati ya sababu ambazo zimemfanya aachane naye.

Pamoja na hayo lakini amesisitiza kuwa wanamahusiano mazuri na wanaongea. "Mimi na Barnaba tunaongea mara kwa mara na yeye ndiye aliniletea mwaliko, Mimi na yeye hatujarudiana lakini ni wazazi na tunashauriana na kuna siku pia aliniita nikasikilize baadhi ya nyimbo kabla album haijatoka''. TOA MAONI YAKO HAPA

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.