Header Ads

Mama wa Miss Tanzania afunguka mapya


Baada ya kuibuka mijadala mingi kuhusu zawadi aliyopatiwa mshindi wa taji la Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth, mama mzazi wa mrembo huyo Esher John Kiloba amedai ndoto ya mwanae kuvaa taji hilo ilianza kipindi akiwa na umri wa miaka minne. 

Bi. Esher ameeleza hayo alipokuwa anazungumza na BIG CHAWA iliyopo ndani ya kipindi cha PLANET BONGO  inayorushwa na East Africa Radio, mara baada ya mtoto wake kushinda taji hilo ambalo lilikuwa linagombewa na washiriki takribani 20 kwenye mashindano yaliyoandaliwa na Bi. Basila Mwanukuzi. 

"Harakati za mwanangu alianza akiwa mtoto wa miaka minne tu, siku ya kuzaliwa Quen Elizabeth alikuwa anataka avae 'crown', alikuwa hawezi kula keki bila ya kuvaa 'crown' kabisa. Niliweza kumruhusu mwanangu kushiriki mashindano haya kwasababu ni mtoto ambaye anajitambua katika kile anachokifanya", amesema Bi. Esher. 

Kwa upande wake, Queen Elizabeth amesema alikuwa anategemea kushinda taji hilo kwa mwaka huu, huku akidai mipango aliyokuwa nayo kwa sasa ni kutaka kuitumikia jamii ya Watanzania katika masuala mbalimbali. 

Kabla ya kushinda taji la Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth ameshawahi kushinda taji la  Miss Kinondoni 2018, Miss Dar es Salaam 2018. 

Queen Elizabeth Makune ana umri wa miaka 22 na kwa sasa ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania, (TIA), akichukua Shahada ya Kwanza ya Uhasibu na Fedha.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.