Header Ads

Mambo ya kuzingatia ili ujue namna ya kumiliki pesa


Wakati mwingine ni bora tuwe wakweli katika somo linalohusu pesa kwani ndilo  somo ambalo watu wengi hufeli sana hasa pale wanapozipata, wapo baadhi ya watu wakizipata  pesa hujikuta  hawana kitu au zimeisha pasipo kufanya mambo ya msingi.

Wengi wao wamesahau ya kwamba pesa zina kanuni na misingi yake  ambapo kila mwenye kuzihitaji ni lazima aweze kuzielewa kanuni hizo, na pia kanuni hizo ni lazima aendane na misingi pamoja na nidhamu ili ziweze kujizalisha.

Hivyo ili uweze kumiliki pesa unatakiwa kufahamu mambo haya ya msingi yahusuyo pesa kama ifuatavyo:-

1. Ongeza kiwango cha uzalishaji.
Ukitaka kuishi katika kiwango kizuri cha umiliki wa pesa unatakiwa kuzingatia misingi itayokusaidia wewe kuweza kuwa hivyo, na miongoni mwa kitu kitakachokusaidia kuweza kuishi hivyo unatakiwa kila wakati kujifunza kupanua wigo wa uzalishaji na usambazaji wa huduma unayoifanya, huku ukizingatia kuzalisha bidhaa yenye ubora wa hali ya juu sana kadri uwezavyo.

Kitendo cha kufanya hivyo kitakusaidia sana kuweza kupata wateja wengi sana huku na wewe kwa upande wa ‘wallet’ yako ukiwa unazidi kunona kila wakati.

Kanuni hii inakutaka sana wewe kufahamu ya kwamba kama ulikuwa unazalisha kwa kiwango cha hatua tatu basi jitahidi kuongeza kuzalisha walau kwa hatua sita za ziada, kufanya hivo kutasaidia kwa kiwango fulani kuweza kupiga hatua za kimafanikio.

Angalizo kuhusu njia hii ni: kabla hujaongeza kiwango cha uzalishaji na usambazaji angalia tabia ya walaji wako, kama kuna ongezeko la wateja basi  njia hii itasadia ila kama kuna upungufu wa walaji au wateja basi njia hii haitafaa.

2. Fanya uwekezaji.
Moja kati ya kununi mojawapo inayowaathiri watu wengi walipo kwenye maisha ya kawaida ni kwamba wao huishi katika kanuni za kilevi yaani hatua tano anakwenda mbele harafu anarudi nyuma hatua kumi, hii nikiwa na maana ya kwamba wao mara baada ya kupata pesa wamekuwa wakizitumie pesa hizo kuliko kufanya uwekezaji.

Hivyo kanuni nyingine ya muhimu unayopaswa kuifahamu kuhusu pesa ni kuifanya pesa ijizalishe yenyewe kuliko kuwa na matumizi yasikuwa ya lazima. Hii ikiwa na maana ya kwamba kwa kila kitu unachokifanya hakikisha kila ukipata pesa unatakiwa kuifanya pesa hiyo ijiongeze.

Kanuni ya kufanya hivyo ili iweze kuitimia, kwanza unatakiwa kupanga mipango yako ya kiutendaji kabla pesa hiyo haijakufikia. Kufanya hivyo kutasaidia kuondokana na ile dhana kwamba kupata pesa ni zari, na dhana hii ukiwa nayo itakufanya mara baada ya kuapata pesa utakuwa ni uwekazaji kuliko kuwa mtu wa matumizi yasiyokuwa ya lazima.

Hivyo kila wakati ni lazima uweze kuelewa ya kwamba kanuni ya pesa inasema Mipango+pesa+uwekezaji=mafanikio, kanuni hii pindi utakapoiweka katika fikra na akili yako itakusaidia sana kuweza kuishi maisha ya hulka ya kuwa na nidhamu katika pesa.

Hivyo kila wakati ili uweze kufanikiwa katika kipengele cha umiliki wa fedha unatakiwa kufahamu ya kwamba pesa yeyote unayoipata tenga silimia kadhaa katika uwekezaji , hii itakusaidia sana kuifanya pesa hiyo ijizalishe yenyewe

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.