Header Ads

Mbunge CCM aibua sakata la Richmond Monduli


 Mbunge wa Ulanga (CCM),Goodluck Mlinga amewataka wakazi wa Monduli mkoani Arusha kumuuliza waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa sababu za kujiuzulu baada ya kuibuka kwa sakata la  Richmond.
Mlinga ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Septemba 8, 2018 katika mkutano wa kampeni jimbo la Monduli uliofanyika eneo la Mukuyuni.
Amesema Lowassa anamshambulia mgombea wa CCM katika jimbo hilo, Julius Kalanga kuwa amejiuzulu uanachama wa Chadema na kuhamia chama tawala kwa sababu alikuwa na deni la Sh600milioni, wakati yeye alijiuzulu uwaziri mkuu kwa kuchukua fedha za Richmond.
Waziri huyo mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, amekuwa hazungumzii sakata hilo la Richmond na inapotokea kulizungumzia amekuwa akieleza kuwa alijiuzulu kisiasa kuilinda Serikali ya CCM na kwamba ushiriki wake ulitokana na maagizo kutoka juu.
Kampuni ya Richmond Development Company ya Marekani ilipewa zabuni ya kufua umeme wa dharura wakati nchi ilipokuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa nishati hiyo mwaka 2006.
“Jamani kati ya anayedaiwa na ambaye amejiuzulu kwa tuhuma za kuchukua fedha za umma nani bora,” amehoji Mlinga.
Mlinga amesema watu wengi wamekopa na kudaiwa lakini sio tatizo kwa kuwa anayekopa hulipa, deni halifungi mtu.
Amewataka wakazi wa Monduli kupuuza tuhuma kuwa Kalanga alijiuzulu ili kulipiwa deni kwani kauli hizo ni za kisiasa.
Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda aliwataka wananchi kuchagua mgombea wa CCM kwani ndio atawaletea maendeleo.
"Kama mnataa maendeleo mchagueni Kalanga lakini kama mnataka  kujaza nafasi basi chagueni wengine,” amesema.
Amesema  jimbo hilo lipo wazi lakini Serikali inaendelea kusaidia na akichaguliwa Kalanga atasaidia zaidi kwa sababu anaunga mkono Serikali ya CCM.
Mbunge wa Mbulu Vijijini, Fratei Massay amesema wakazi wa Monduli kama wanataka maendeleo lazima wamchague Kalanga.
Amesema Monduli ina historia kubwa katika Taifa na miaka yote ilikuwa CCM lakini wengi walihamia Chadema akiwepo Kalanga kutokana na kile alichokiita kimbunga.
"Kile kimbunga kimepita amerudi nyumbani na kama tunataka Rais afurahi na aje kututembelea mchagueani Kalanga,” amesema.
Soma Zaidi:

    Get it on Google Play

    No comments:

    Powered by Blogger.