Header Ads

Mfahamu John MacCain Aliye kuwa wa mkosoaji mkubwa wa mwendendo wa Rais TrumpKwa sasa jimbo la Arizona lipo katika majonzi makubwa baada ya kuondokewa na seneta wake kipenzi, aliyekuwa alama yao ya ushindi, John McCain. Ilikuwa Agosti 25, 2018 taarifa zilipoenea kuhusu kifo cha mpambanaji huyu wa Marekani. Alipambana na kujitoa kwa ajili ya Marekani kuanzia akili mpaka nguvu zake.
Tunamzungumzia John ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa mwenendo wa Rais wa Marekani, Donald Trump. Kumbuka hakuwa adui wa Trump mahala pengine isipokuwa katika siasa na aina ya sera za zake.
Ili kuuonyesha ulimwengu kwamba yeye ni hasimu m kubwa wa Rais Trump na pengine wasingekuja kuelewana, John Mcain aliwaambia marafiki na familia yake kwamba Rais huyo asikanyage kwenye msiba wake.
Unajua kwanini? Chokochoko zilianza mwaka 2015 katika uteuzi wa mgombea wa urais kupitia Republican na wakati wa kampeni za urais mwaka 2016. MacCain alimuunga mkono Trump kwa nguvu zake zote lakini mambo yaligeuka pale Trump alipotumia kisa cha MacCain kukamatwa Vietnam mwaka 1967 kama fimbo ya kumchapia.
Trump alisema “MacCain ni shujaa wa vita kwa kuwa alikamatwa. Napenda watu ambao hawakukamatwa.” Mambo hayakuishia hapo kwani baadaye kulifichuka nyaraka za sauti zikimhusisha Trump na udhalilishaji wa wanawake na MacCain akajitoa.
Chokochoko ziliendelea mpaka wakati wa kupigia kura muswada wa aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama ambapo Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter “tuiangushe Arizona” kwani MacCain akiwa seneta wa Arizona aliuunga mkono muswada huo huku Trump akiupinga.
Katika mahojiano na chombo kimoja cha habari MacCain aliulizwa ikiwa ni kweli aliunga mkono muswada wa Obamacare kutokana na ujumbe wa Trump.
Alisema “yeye (Trump) anafanya biashara na amefanikiwa katika televisheni na hata warembo wa Marekani, na wengine. Nililelewa katika familia ya kijeshi yenye imani, heshima na nidhamu ambayo taifa letu linapaswa kuiheshimu kila siku.”
Vilevile sera za Trump dhidi ya mataifa mengine kama ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico na sera dhidi ya wageni ni mambo ambayo yalimchukiza sana MacCain.
Mambo haya yalimfanya MacCain kuandika kitabu kilichochapishwa Mei 2018, The Restless Wave ambacho licha ya kuzungumzia maisha yake pia ameelezea utawala wa Trump. Katika moja ya kurasa za kitabu hicho, MacCain anamkosoa Trump akisema “…hana huruma kwa wakimbizi, wasio na hatia, anawasumbua wanawake, wanaume na watoto ambao wameteseka na kukataa tamaa…anavyoongea na kuwachukulia utadhani maisha mazuri au ugaidi ni jambo pekee linalowaleta nchini mwetu.” Hizo ni miongoni mwa sababu za kuwa na uadui mkubwa wa kisiasa kati ya MacCain na Trump.
Alilitumikia jeshi la Marekani katika nyadhifa mbalimbali, ikiwamo ya urubani ambayo aliitumikia kwa muda mrefu zaidi.
Alilitumikia jeshi kwa zaidi ya miaka 18 kabla ya kuanza siasa mwaka 1980. Alitunukiwa nishani kadhaa za jeshi za nyota, fedha, shaba na nyinginezo. Aliachana na jeshi mwaka 1981 alipoamua kujihusisha na siasa.
Moja kwa moja John alijitosa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea useneta katika Bunge la Congress kwa tiketi ya Republican.
Kwa kuwa alikuwa kijana maarufu na shupavu, haikuwa vigumu kwake kushinda kwani aliingia bungeni kwa mara ya kwanza kuliwakilisha jimbo la Arizona mpaka alipofariki dunia.
Alizaliwa katika familia ya kijeshi ya John S. JR. Alikuwa mwanajeshi na rubani katika jeshi la Marekani na kushiriki katika vita mbalimbali vya Marekani dhidi ya mahasimu wake. John alikuwa na moyo wa uzalendo na kujitoa kwa nchi yake tangu akiwa kijana mdogo. Uzalendo huu ndio uliomfanya aamue kujiunga na kambi ya mafunzo ya jeshi la maji la Marekani iliyopo Annapolis, Maryland.
Kibarua chake kikubwa kilikuwa mwaka 1967 ambapo alikuwa kikosini kama rubani wa ndege ya kivita katika vita ya Marekani na Vietnam. Wakati vita vimepamba moto, ndege yake ilitunguliwa na vikosi vya Vietnam, Oktoba 26, 1967 akamatwa mateka na kuswekwa ndani.
Baada ya kukamatwa, MacCain alipelekwa katika kambi ya Hanoi Hilton ambako alipata mateso ya kila aina. Alivunjwa kuvunjwa mguu, mikono, bega na kupata majeraha mengine makubwa. Miaka mitano na nusu baadaye, yaani mwaka 1973 aliachiwa huu baada ya makubaliano ya amani ya Paris.
Mwanzoni kabisa niliuliza kwanini John MacCain atakumbukwa na WanaArizona, Wamarekani au dunia? Si jambo la kushangaza kumuona MacCain akiwa maarufu wakati huu akiwa marehemu pengine kuzidi wakati mwingine wowote.
MacCain alikuwa mzalendo kwelikweli, aya chache zilizopita hapo juu nimeeleza kuwa MacCain alitoka katika familia ya kijeshi, yaani babu pamoja na baba yake mzazi (Sidney MacCain) walikuwa wanajeshi. John MacCain alichagua kujiunga na jeshi si kwa sababu ya shinikizo la wazee la hasha, John alikuwa na mapenzi makubwa na nchi yake. Hakukubali kuwaona maadui wa Marekani wakiwa hai. Mtu au taifa lolote ambalo lingeenda kinyume na maslahi ya nchi yake ilikuwa kinyume naye.
Hata baada ya kukamatwa huko Vietnam baada ya ndege yake kututunguliwa, akateswa na kufungwa kwa miaka zaidi ya mitatu, John alitibiwa na kuendelea kulitumikia jeshi la Marekani mpaka mwaka 1981 alipostaafu rasmi kama kiongozi wa marubani. MacCain alikuwa tayari kufa kwa ajili ya nchi yake. MacCain anatuonyesha njia na maana ya uzalendo hasa. Vijana na watu wengapi wapo tayari kuitetea nchi yao mpaka kufa? Nchi nyingi duniani hasa Afrika zimekuwa na vijana ambao wapo tayari kuiuza nchi yao kwa sababu ya maslahi yao binafsi na wala sio kwa ajili ya nchi.
Kumbuka MacCain hakujiunga na jeshi kwa sababu ya ukosefu wa ajira au umaarufu kwa kuwa tayari familia yake ilikuwa na umaarufu mkubwa na pesa zilikuwepo. Mapenzi na nchi yake yalimfanya ajiunge na kwa ajili ya kulilinda taifa lake.
Kugombea urais
MacCain anajipambanua na wanasiasa wengi kuhusu dhamira ya uongozi. Alianza kukiwania kiti cha urais wa Marekani mwaka 1999. Kwanza ilibidi ashinde katika kura ya maoni katika chama chake cha Republican ambapo hata hivyo hakufua dafu mbele ya rais wa zamani wa taifa hilo, George W. Bush.
Hata hivyo, mwaka 2007 licha ya kushinda kura za maoni na kuwania kiti cha urais alishindwa kufua dafu dhidi ya rais wa mstaafu, Barack Obama wa Democrat.
Mwaka 2008 John McCain alipokuwa mgombea urais wa Marekani, mgombea mwenza wake alikuwa gavana wa Alaska, mlimbwende Sarah Palin.
Mgombea mwenza huyo mwaka 1984 alishinda mashindano ya ulimbwende ya Wasilla, pia aliwahi kuwa mshindi wa tatu kwenye mashindano ya ulimbwende ya Alaska.
Ujasiri wa kukosoa
Jambo lingine ambalo linamfanya MacCain kuwa mtu wa pekee ni ujasiri wake wa kukosoa na kupinga hadharani bila woga tena kwa hoja madhubuti.
Hivi majuzi
Trump alikutana Rais wa Urusi, Vladmir Putin. Wakati mazungumzo hayo yanafanyika tayari kulikuwa na fukuto la Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani hasa kampeni za Trump ambazo zilimsaidia kushinda urais, hakukuwa na mazungumzo yenye tija kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.
MacCain alipinga vikali mazungumzo hayo akisema “moja ya mambo ya fedheha kabisa kufanywa na Rais wa Marekani katika historia.” Alisema wazi kuwa si tu kwamba Trump alishindwa lakini hakuweza kufurukuta kwa Putin.
Alijitoa kwa ajili ya watu wengine, si tu kwamba MacCain alitoa mhanga kwa ajili ya taifa lake bali alijitoa hata kwa mtu mmoja mmoja.
Moyo wa kujitoa
Kutoka mwaka 2001-2006 MacCain alikuwa ametumia kiasi cha dola za Kimarekani faidi ya 950,000 kwa ajili ya kusomesha watoto katika shule mbalimbali kupitia mfuko wake wa The MacCain Foundation ambao mkewe ni mwenyekiti.
MacCain hakujisikia vibaya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya watu wengine. Ni watu wangapi ambao leo hii wanaweza kutumia mamilioni kusomesha watoto na kuwapa mahitaji mengine barani Afrika?
Ni watu wangapi tunawafahamu wanatumia fedha walizonazo kwa mambo ambayo hayana umuhimu wakati nchini yetu ina maelfu ya watoto wasio na mahitaji?
Mwandishi ni mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Kiswahili katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
0672395558

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.