Header Ads

Mkuu wa wilaya babati akabidhi pikipiki 11 kwa vijana


Mkuu wa Wilaya wa Babati  Mhe. Elizabeth Kitundu amekabidhi pikipiki 11 kwa vijana 11 zenye thamani ya shilingi milioni 23,200,000, ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu  kutoka Mabadiliko Saccos Ltd utakaowawezesha  vijana wa kundi hili kujiajiri na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira pamoja na umasikini.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo Mhe Kitundu amesema kuwa vijana wengi wamekua wakikabiliwa na tatizo la mtaji hivyo pikipiki hizo zitawasaidia kukuza mitaji yao na kuongeza kipato chao cha kila siku na kuondokana na umasikini huku akiwasisitiza kujiunga na mfuko wa Bima ya afya ili kupunguza gharama kubwa za matibabu.

 Aliongeza kuwa “Vijana hao wamekuwa wakipata Pikipikizi hizi kwa gharama kubwa zaidi kutoka kwa wamiliki binafsi ambapo inapaswa kulipa mara mbili ya bei ya Pikipiki ndipo unaweza kumiliki au aendelee kurejesha Fedha siku zote mpaka Pikipiki itakapokufa hivyo kunufaisha watu wachache ilihali wao wakiendelea kuwa na hali duni kimaisha”.

Katibu wa bodi ya  Mabadiliko Saccos Hussen Suleimani anasema kwa sasa wameanza kutoa mikoipo hiyo kwa vijana na wanafanya mpango wa kuwasaidia walemavu kupata mikopo hiyo kama alivyosisitiza mkuu wa wilaya Elizabeth Kitundu.

Vijana walionufaika na mkopo huo wa piki piki wameeleza kuwa watakuwa tayari kujituma ili kuweza kurejesha maresho na kuongeza kuwa itakuwa ni nafuu kwao kwani walikuwa wakinyanyaswa na wenye piki piki kwa kurejesha 10,000 kwa siku hali ambayo ilikuwa  ikiwapa ugumu kupata fedha hizo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Boda boda Mkoa wa Manyara Musa Mnyamu  amewataka vijana hao kuzitunza piki piki hizo na kutii sheria bila shuruti,kuvaa kofia ngumu na kuendesha wakati wapo timamu bila kunywa pombe.

Naye mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika  mkoa wa Manyara  Venance Msafiri amewataka vijana hao wazitumie pikipiki walizopatiwa katika kuwaingizia kipato,isiwe chazo cha ajali kwa kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuinua vijana kiuchumi ili kuwa na taifa imara.

Hivyo  vijana hao watapaswa kurejesha Tsh 7,500 kwa siku 365 sawa na Tsh milioni 30,112,500  na watamilikishwa Pikipiki hizo kuwa zao

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.