Header Ads

Mtu mmoja Wilayani Bahi Mkoani Dodoma Akutwa Amejinyonga kwa sababu zisizo julikana

DODOMA:Mkazi mmoja mwenye umri wa miaka 50,wa kijiji cha babayu msangani Wilayani bahi mkoani Dodoma, amekutwa amejinyonga kwa sababu ambazo hazikujulikana mara moja.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akiongea na Maisha fm kwa njia ya simu mwenyekiti wa kijiji hicho bw Jumanne Mohamed Seleman,amesema kuwa tukio hilo limetokea sept 10 mwaka huu majira ya saa tatu asubuhi ndipo mwili wa marehemu Aliyejulikana kwa majina ya Mohamed Yahya Nduli ,ulipokutwa ukining’inia kwenye tawi la mti shambani na chini yake kukutwa ujumbe umeandikwa kwenye kipande cha karatasi ukiwaelekeza mahali makumzika.

Naye shuhuda wa tukio hilo ambae ni kaka wa marehemu anayejulikana kwa majina ya Sumbwi Lungwa Mduli  ameelezea masikitiko yake na namna tukio lilivyotokea huku akisema kuwa marehemu hakuwa na ugomvi na mtu yeyote wala familia.

Hatahivyo mwenyekiti  wa kijiji hicho amewataka wananchi kuacha kuchukua maamuzi ya na mna hiyo kwani sio sahihi na badala yake watafute njia mbadala ya kutatua matatizo yanayo wakabili hususani kisaikologia.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.