Header Ads

Serikali kushusha neema kwa wanafunzi wenye ulemavu


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Stela Ikupa amesema serikali imeanza kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na wadau mbalimbali wa elimu yakiwemo ya walimu kujua lugha ya alama kufuatia wanafunzi wa shule ya viziwi Njombe sekondari kufeli darasa zima kwa kupata sifuri katika mitihani yao ya kidato cha nne 2017.

Akizungumza na Wandishi wa habari Naibu Waziri Ikupa amesema kuwa kati ya mapendekezo ambayo serikali imeanza kuyafanyia kazi ni pamoja na kuanzisha mtaala maalum kwajili ya kufundisha walimu lugha ya alama ambayo ndiyo inatumiwa na viziwi.

Baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya katiba na sheria wamesema kuwa serikali inatakiwa kupata idadi kamili ya walemavu waliopo nchini ili kuweza kupanga bajeti itakayoweza kulifikia kundi na kuhakikisha wanapata haki zao za msingi

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.