Header Ads

Serikali yatoa maagizo kwa walimu watako kiuka sheriaMdhibiti Mkuu wa Ubora wa shule kanda ya kaskazini Magharibi Victor Bwindiki  amesema serikali haitamvumilia  mwalimu atakayetoa  adhabu itakayojeruhi au kukatisha uhai wa mwanafunzi kwakuwa walimu  wanatakiwa kufanya kazi  kwa kuzingatia nguzo tano za ualimu  na kuwa  makini katika  utoaji  wa adhabu itakayochafua taswira ya ualimu na kukatisha ndoto za mwanafunzi.

Bwandiki amesema hayo alipokuwa anazungumza na walimu, wanafunzi na wazazi na kusema kuwa  baadhi ya walimu wamekuwa wakimalizia hasira za  matatizo ya familia zao kwa  wanafunzi bila kujali utu wa wanafunzi " Serikali kamwe hatamvumilia mtumishi wa aina hiyo bila kujali kuwa ni wa shule ya serikali au binafsi kwakuwa zote zipo chini ya serikali," alisema.

Mwalimu Mkuu  wa shule ya Msingi Holly Peak Sophia Abdulsaboor amesema mwalimu anapaswa kuwa rafiki na  mwanafunzi ili  aweze kumwandaa kufanya vizuri kitaaluma  na  hakuna ulazima wa kutumia nguvu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.