Header Ads

Simba yalazimika kuondoka na alama 1 dhidi ya Ndanda fc

Klabu ya Simba imelazimika kuondoka na alama moja dhidi ya Ndanda Fc katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Nagwanda Sijaona, mkoani Mtwara.

 Katika mchezo huo ambao ni wa tatu kwa Simba na wa kwanza kwa klabu hiyo kucheza ugenini msimu huu, umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bila kufungana.

Kwa sare hiyo, Ndanda Fc inaweka historia ya kuondoka na alama katika mchezo wake wa nyumbani dhidi ya Simba, baada ya kufungwa kwa misimu mitatu tangu ilipopanda daraja kwa mara ya kwanza msimu wa 2015/16.

Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa hii leo katika viwanja mbalimbali ni, JKT Tanzania iliyoibuka na ushindi ugenini wa 1-0 dhidi ya Mbao Fc, Singida United nayo ikiibuka na ushindi ugenini wa 1-0 dhidi ya KMC, Tanzania Prisons ikitoka sare ya 2-2 na Ruvu Shooting na Biashara United ikitoka sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar.

Simba sasa inafikisha alama saba sawa na Azam Fc, Mtibwa Sugar, Mbao Fc na Singida United

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.