Header Ads

TAKUKURU Mkoani Manyara yapokea taarifa za rushwa 315

 Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Manyara imesema kwa mwaka 2018 pekee imepokea taarifa za rushwa 315  kutoka kwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa Habari  Naibu mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Isdory Kyando amesema kati ya hizo 154 hazihusiani na Rushwa,161 zilikuwa za rushwa moja kwa moja ambapo kati hizo 34 zilifanyiwa uchunguzi wa kina na kupeleka majalada  kwa mkurugenzi wa Mashtaka.

Aidha Kyando amesema  kwa mwaka huu na mwaka jana   wamefungua kesi  26 mahakamani ambayo ni idadi kubwa ukilinganisha na mwaka jana kesi 15 ambayo inafanya jumla kuwa  kesi 41 ambapo kati ya hizo 15 zimeshatolewa maamuzi na mahakama,kumi washtakiwa wamepatikana na hatia  ambayo ni zaidi ya asilimia 66% na kesi tano washtakiwa wameonekana hawana hatia.
Amesema Serikali za vijiji na mitaa zinaongoza kulalamikiwa kupokea rushwa ambapo wamepokea taarifa 47,ya pili ni idara ya polisi mkoa taarifa 42,ya tatu  taasisi binafsi 31,ya nne mabaraza ya kata 31 ,ya tano ni taarifa binafsi 18 na  ya sita ni mahakama malalamiko 11.

Aidha Kyando ameeleza kuwa Kama kila taasisi itakuwa na mfumo mzuri wa kujidhiti wenyewe itapunguza tatizo la rushwa kwa kiasi kikubwa na jukumu la TAKUKURU halitakuwa kubwa kama ilivyo sasa.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.