Header Ads

Uwoya afungukia madai ya kuwa na mpenzi Dubai


WATU wengi wanajua ubuyu wenye ladha ni ule mwekundu tu, lakini siyo kweli kwani kuna ubuyu mwingine mweupe, blu na hata kijani na yote ina ladha moja!  Ubuyu uliotua mezani kwetu wiki hii unadai kwamba staa mwenye mvuto wa kipekee Bongo Muvi, Irene Uwoya, juzikati alikuwa anatanua huko Dubai na mwanaume mwingine tofauti na mumewe ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’. Chanzo chetu kilichomwaga ubuyu huo kilidai kuwa, Uwoya na Dogo Janja hawana maelewano tena ndani ya ndoa yao hivyo mwanamama huyo alikwenda kupumzisha akili yake huko.


huku ikidaiwa ameambatana na mwanaume huyo mwingine. “Uwoya ameona kama haelewi kabisa kuhusiana na ndoa yake na ni kama haipo kabisa ndiyo maana aliamua kuondoka kwenda kutuliza akili nje ya nchi. “Lakini ilidaiwa huko alikwenda na mtu mwingine mwenye pesa zake nyingi tu,” alisema mtoa ubuyu wetu.

MSIKIE UWOYA MWENYEWE HAPA
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, kama ilivyo desturi yake, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Uwoya ambapo mambo yalikuwa hivi;

Ijumaa Wikienda: Mambo vipi, mzima?

Uwoya: Mzima, niambie.

Ijumaa Wikienda: Kuna ubuyu hapa kuwa ulikwenda Dubai na mtu mwingine na siyo Dogo Janja, je, ni kweli?

Uwoya: Jamani kwani kila sehemu ninatakiwa niwe naye? Hata kama nipo kikazi?

Ijumaa Wikienda: Mbona unaonekana kwenye picha mbalimbali kama ulikuwa unajirusha tu?

Uwoya: Hivi mtu anaweza kujua mambo yote ya mtu kupitia picha zake anazoposti tu ndiyo akaanza kumjadili na kujijibu maswali yote? Ni ngumu kumueleza kila mtu mambo yako.

Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo huko ulikwenda kufanya nini?

Uwoya: Kupumzika, tatizo Wabongo mtu akiamua kwenda sehemu nzuri, basi utasikia amelipiwa, kwa nini jamani? Tunapaswa kubadilika, nimetumia pesa zangu kujipa amani na furaha.

Ijumaa Wikienda: Mbona tunasikia ulikwenda na mtu ndiye anakupa raha zote hizo sasa hivi?

Uwoya: Ndiyo maana nikakuambia hatuwezi kuendelea kwa kufikiria kwamba mtu hawezi kufanya kitu mwenyewe mpaka alipiwe na mtu!

Ijumaa Wikienda: Nakushukuru Uwoya kwa ushirikiano.

Uwoya: Asante

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.