Header Ads

Wadau Tumsaidie Hawa wa Nitarejea ya Diamond...Diamond Platnumz Funguka Roho BabaMiaka kadhaa iliyopita niliposikia wimbo wa NITAREJEA nilikubali kuwa ni wimbo bora na umebaki kuwa bora kwa wakati wote, Hauchuji, haufubai, haupitwi na wakati. Ni wimbo wenye ujumbe mzuri na uliojaa hisia.

Producer aliyehusika aliutengeneza vizuri na waimbaji (Diamond na Hawa) waliunogesha kwa sauti maridhawa.

Japokua Hawa alikua chipukizi lakini aliimba kwa ustadi mkubwa, na wengi walitegemea angepaa kimuziki kuanzia pale. Bahati mbaya mambo hayakwenda kama ilivyotarajiwa. Amepitia mitihani mingi mikubwa ya maisha iliyomkwamisha huku Diamond akipaa Kimuziki

Aliolewa na mumewe kumkataza kujihusisha na muziki. Kwa kuheshimu ndoa na kulinda familia yake alikubali. Akapata mimba na kujifungua lakini mumewe akaondoka akidai kwenda kutafuta maisha, Hakurejea.

Kuanzia hapo akaanza kuhangaika ili aweze kuendesha maisha. Alipe nyumba, umeme, maji, chakula, mavazi na malezi ya mwanae.

Akiwa katika msongo mkubwa wa mawazo akajikuta ameangukia kwenye ulevi wa kupindukia wa pombe kali aina ya Gongo. Akadhoofu mwili. Lakini baadae alisaidiwa akaacha.

But imegundulika ameathirika ini kutokana na pombe kali, hivyo anahitaji kufanyiwa liver transplant. Hana uwezo wa kwenda kupata matibabu nje ya nchi. Muhimbili wanamsaidia tu kunyonya maji yaliyojaa tumboni hadi atakapopata msaada wa kufanyiwa Liver transplant.

Katika umri mdogo Hawa amepitia mambo mengi mazito, hata hivyo amejikuta akipambana peke yake. Mwaka jana alipoachana na pombe aliomba Diamond amsaidie aweze kurudi kwenye sanaa, lakini hakumsaidia. Anasema hata simu zake hakupokea. Alijaribu kutoa wimbo mmoja lakini haukuwika sana. Diamond alihojiwa na media hakujibu vizuri

Kwa sasa yupo kitandani akiugulia maumivu makali ya ini. Naomba tumsaidie. Pia mwambieni Diamond kuwa kama alishindwa kumsaidia kurudi kwenye sanaa basi angalau amsaidie kupata matibabu. Bado anamsubiri arejee kama alivyoahidi kwenye wimbo wake.

Hawa ni moja ya single mamaz wengi wanaoteseka kwa sababu ya kutelekezwa na wanaume zao.

Plz letz save this inocent soul.

Wasiliana na mama yake mzazi kupitia 0712032705 au 0762313587. Unaweza kumpigia kwanza ili kujiridhisha. Mungu akukubariki #AMEN

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.