Header Ads

Wadau wataka kiswahili kifundishwe ngazi zote


mwalimu
Lugha ya Kiswahili ndiyo lugha kuu ya kwanza ya taifa nchini Tanzania, ndiyo lugha inayozungumzwa katika eneo kubwa la bara la Afrika, ikiwa na wazungumzaji zaidi ya 100 millioni huku ikitajwa kuwa ni miongoni mwa lugha inayokua kwa kasi hivi sasa duniani.

Mafanikio hayo yote hayajaifanya lugha hiyo adhimu kuanza kutumika katika ngazi mbalimbali za elimu nchini hasa kuanzia ngazi ya sekondari, kwani mpaka hivi sasa lugha ya kiswahili inatumika kufundishia ngazi ya shule za msingi pekee.
Utafiti mwingi unaonesha wanafunzi wengi wanaomaliza shule za msingi hupata wakati mgumu wanapojiunga na sekondari kwasababu ya matumizi ya lugha ya kiingereza katika msomo yao ilihali wakiwa wamezoea lugha ya kiswahili waliyoishi nayo kwa miaka saba katika shule za msingi.
Kupitia kipindi cha funguka kinachoruka kupitia EATV na katika ukurasa wa Facebook tunaruhusu wadau kuchangia mada mbalimbali, ambapo hii leo tumeweka mada iliyouliza “Unadhani NECTA wakiruhusu watu kujibu mtihani kwa kiswahili itaongeza ufaulu ?, na haya hapa ni baadhi ya maoni ya wachangiaji wa mada hiyo.
Halima Bamhiga:  wa Mlandizi, Kibaha Pwani, kwa mtazamo wangu naona itaongeza ufaulu kwa kiasi fulani sababu kiswahili ndio lugha tulioizoea, ni lugha mama.
Ombeni Eliewaha:  wa Monduli, Arusha, kwa mimi naona itasaidia kwa sababu mtu unakuta anajua jibu lakini hajui kujibu kwa kiingereza. Pamoja sana ndani ya show mpaka tamati, hivo yaani.
Twaib Mswadiku: wa Chato, Geita #funguka, mimi naona kiswahili kutumiwa kama kujibia mitihani haitasaidaia chochote hapo maana kiswahili kina misamiati migumu halafu ni mingi, mfano kudamshi wakati kwenu English ni ‘beulfull’.
Maria Mutondi: Kama wamewafundisha kiswahili toka mwanzo wakijibu kwa kiswahili ni sawa ila kama waliwafundisha kiingereza basi wajibu kwa kiingereza. Pia lazima kujua kuna wanafunzi waliosoma English mediums.
Hamis Hashim: Kingereza chenyewe kinafundishwa kwa kiswahili, ili ujibu swali lazima ubadili swali kutoka kingereza kwenda kiswahili, sasa kwanini wanafunzi wasifauli kwa kutumia lugha yao adhimu ya kiswahili???. Nasema watafaulu bila shida ukitaka kuamini jiulize kwnini shule za msingi watoto wengi wanafaulu hasa masomo yanayofundishwa kiswahili.
Sanga Feician Junior: Kama somo la kiswahili wanafunzi wote nchini wangekuwa wanapata daraja "A" hapo ingekuwa sawa . Pia mitihani ya shule za msingi inatungwa kwa lugha mama na bado wanafunzi tunafeli, suala tupambane kwenye nyenzo za kufundishia na wanafunzi wajitambue nini wanafanya.
Kati ya wachangiaji takribani 200 wa mada hiyo, ni wachangiaji 34 ndiyo waliopinga kuwa haitosaidia katika ufaulu wa wanafunzi huku wachangiaji saba wakisema hawajui.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.