Header Ads

Waitara ataja sababu zitakazo mfanya kuibuka mshindi ni hizi


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mwita Waitara amezungumzia juu ya muamko hafifu wa upigaji kura katika Jimbo hilo changamoto ambayo pia ilitajwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jumanne  Shauri.

Akizungumza na www.eatv.tv Mwita Waitara amesema huenda kuna sababu mbalimbali zilizopelekea muamko hafifu na kuwataka wananchi kujitokeza kabla ya saa kumi ili kupiga kura.

"Wananchi wanajua zoezi linaisha saa kumi jioni, kuna wengine wanashughuli mbalimbali mi naona zoezi linaenda vizuri hali ni shwari na bado kuna muda wa kutosha wa watu kuendelea kupiga kura..." amesema Waitara

Katika hatua nyingine Waitara amezitaja sababu zitakazomfanya  kuibuka kinara wa uchaguzi wa marudio.

"Unajua siasa nimefanya muda mrefu na watu wa Ukonga nimeishi nao vizuri, Tangu niliposimamishwa nilijua naenda kushinda kwa kuwa Mpinzani wangu pia sio mkazi wa Ukonga.." ameongeza Waitara

Uchaguzi wa jimbo la Ukonga unarudiwa kufuatia aliyekua Mbunge wa jimbo hilo kupitia CHADEMA Mwita Waitara kutangaza kujivua nafasi hiyo july 28 mwaka huu kwa madai ya kuwa na mgogoro na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.