Header Ads

Yanga yakusanya zaidi ya milioni 30 kwenye harambee yao


Licha ya watani zao wa jadi Simba kuwapiga majungu baada ya kuanzisha harambee ya kuomba michango ya fedha ili kuipa nguvu klabu, imeelezwa fedha hizo zimeanza kuweka mambo sawa katika klabu ya Yanga.

Taarifa zilizo ndani ya uongozi wa Yanga zinasema kuwa mabosi wa timu hiyo wamefurahia mchango ambao unazidi kutolewa na wanachama wake ambao umekuwa ikiipa sapoti timu yao mpaka sasa.

Yanga imekusanya kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 30 kwa mwezi uliopita ambazo zimekuwa chachu ya mafanikio tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo maalum.

Unaambiwa fedha za wanachama wa klabu hiyo wenye mapenzi ya dhati na timu imesaidia pia harakati za kuisaifirisha timu kuelekea Rwanda kwa ajili ya kukipiga na Rayon Sports kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Kutokana na kuleta manufaa ndani ya klabu, fedha hizo sasa zinawapa majibu watani zao wa jadi Simba waliokuwa wakikebehi namna walivyoanzisha mpango huo wa kuchngisha fedha.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.