Header Ads

Zahera agoma kuendekeza umaarufu


Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameweka wazi kwamba hataki kuendekeza umaarufu kwenye kikosi hicho na wachezaji wameanza kumuelewa anachomaanisha.

“Kwangu nataka wachezaji wabadilike wajitume na wasifikirie kuwa ukubwa wa majina yao ndiyo nitakuwa nawapanga kwa kila mechi hiyo kitu haipo zaidi nitaangalia kiwango ambacho wanaonyesha katika mazoezi.

“Sababu najua wanatofautiana kwenye viwango sio mmoja kwenye zoezi anafanya kitu mara 10 na mwingine anafanya mara nne na ategemee kwamba nimpange kwenye mechi eti kwa sababu tu ni maarufu hilo walisahau kabisa wanatakiwa kupambana kwa nguvu zote ndipo wataweza kupata nafasi.

“Na pia ninafurahia zaidi kuona wachezaji wanapambana na kuzingatia yale ambayo nawaelekeza wachezaji wangu jambo ambalo litasaidia timu kufanya vizuri msimu huu,”alisema Zahera ambaye aligusia pia mechi ya leo Jumapili dhidi ya Stand.

“Tunakutana na Stand kwa tahadhari kubwa hatuwadharau lakini upande wangu wachezaji wako fiti Kelvin Yondani naye yuko sawa aliumia akiwa na timu ya taifa lakini alifanya mazoezi na sasa yupo vizuri.

“Kitu kingine ninachofurahia ni kupata fursa ya kuweza kukaa benchi wakati ule ilikuwa ni vigumu kutoa maelekezo nikiwa jukwaani kule VIP lakini sasa hivi watakosea nitakuwa karibu kuweza kutoa maelekezo,”alisema Zahera ambaye familia yake iko Ufaransa.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.