Header Ads

Ester Mahawe aiomba serikali kuzungushia ukuta uwanja wa mpira wa kwaraaMbunge  wa viti maalum mkoa wa Manyara Ester Mahawe   ameiomba Serikali, ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Manyara na wadau wa michezo kushirikiana kuzungusha ukuta katika uwanja wa mpira wa Kwaraa wa ili kuweza kuweza kupata mapato kupitia matamasha mbalimbali.

Mheshimiwa Mahawe amesema Matamasha makubwa yanashindwa kufanyika katika mkoa wa manyara kwa sasbabu ya kukosekana kwa uwanja ambao unaweza kukusanya watu wengi akiitaja Fiesta ambayo inaendelea kwa sasa katika mikoa mingine.

Amesema Chama cha Mapinduzi kwa kushirikiana na serikali wapo tayari kuutengeneza uwanja huo uliopo mjini Babati ili kuweza kuzungushiwa ukuta  pamoja na

Wadau mbalimbali wakizungumza na kituo hiki wameeleza kuwa wazo la mbunge huyo likifanyiwa kazi litautangaza zaidi mkoa wa Manyara kupitia matukio makubwa ambayo yatakuwa yakifanyika katika uwanja huo na kuingiza mapato.

Ikumbukwe kwamba Mji wa Babati kwa sasa unakuwa kwa kasi kubwa ndio kitovu cha mkoa wa Manyara tangu uanze miaka kumi na sita iliyopita.

“Watu wa manyara wanazidi kuangalia kwenye televisheni matukio yanayofanyika mikoa jirani kwa sababu ya kukosekana kwa uwanja mzuri,hiin haijakaa sawa”,alisema Mahawe.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.