Header Ads

Hii ndio Sababu kamati kutofanyia miswada marekebisho

BUNGE limesema baadhi ya miswada inayopelekwa kwenye kamati, hupitishwa bila ya kufanyiwa marekebisho kutokana na wabunge wengi kwenye kamati kutokuwa wanasheria.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengelwa, alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la Asasi za kiraia lililoandaliwa na Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kuhusu miswada inayopelekwa bungeni.

Mchengelwa alisema wabunge wengi siyo wanasheria katika kamati hiyo, jambo linalowafanya washindwe kuichambua miswada inayoandaliwa na makatibu na wasaidizi kutoka kwenye kamati.

Alisema mjadala unapofika bungeni hali huwa tofauti kutokana na wabunge wengi kutokuwa wanasheria, hivyo kukosa uwezo wa kuichambua miswada.

“Katika kamati yetu siyo wote wanasheria, baadhi ya wabunge hupitisha kama ilivyoandikwa na makatibu na wasaidizi wa sheria, jambo hilo limekuwa na madhara ingawa kwenye bunge kunakuwa na mivutano mikali,” alisema Mchengelwa.

Katibu Msaidizi wa Bunge Dunford Mpelumbe, alisema milango iko wazi kwa wadau kwa ajili ya kutoa maoni kwenye miswada kabla ya kupelekwa bungeni, lakini alisema mara nyingi watu wanaishia kulalamika nje badala ya kupeleka maoni yao.

Mwakilishi kutoka TlS, Harold Sungusia, alisema kuna changamoto kwa Watanzania kuhusu upelekaji wa maoni kwenye kamati za bunge, jambo linalosababisha vitu vingi kupitishwa bila ya kuwa na sauti za makundi mengine

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.