Header Ads

Jaydee afunguka kuachana na Spice


Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni mkongwe kwenye game na wengi hupenda kumuita dada wa bongo fleva, Lady Jaydee, kwa amefunguka juu ya tuhuma za kuachana na mpenzi wake Spice, ambaye ni msanii kutoka Nigeria Spice.
Akizungumza na mwandishi    www.eatv.tv  Lady Jaydee amesema kwamba hajaachana na Spice, isipokuwa wawili hao wanafanya kazi ambayo inawalazimu kuwa mbali mbali kwa muda mrefu, ikichangiwa na kuwa raia wa nchi mbili tofauti.
Jaydee ameendelea kwa kusema kwamba licha ya Spice kuwa mbali, amechangia kwa kiasi kikubwa kuweza kufanikisha tamasha la #VocalsNight2018, kwa kuweza kumuunganisha na UTI ambaye  alikuwa MC wa siku ile.
“Unajua sisi ni wanamuziki, na wanamuziki ni watu wa kusafiri, na hatuishi nchi moja, kwa hiyo yeye yuko kwenye kazi zake na mimi nipo kwenye kazi zangu, ni sawa na mume na mke, mume anaenda kazini na mke anaenda kazini kwake, haimaanishi kila siku muwe mnafuatana, leo hayuko hapa lakini ni mtu ambaye nashirikiana naye kwenye mambo mengi, kama kunisaidia kumpata UTI na kuhakikisha amefika hapa Tanzania”, amesema Lady Jaydee.
Hivi karibuni kulikuwa na tetesi za wawili hao kuachana baada ya kuwepo ukimya kati yao na kutoonakana pamoja kwa muda mrefu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.