Header Ads

kampuni zinazo toa huduma ya kukusanya na kutupa taka ngumu zatakiwa kuepuka kutupa taka kando ya mito
Dodoma:Serikali imezitaka kampuni  zinazotoa Huduma za kukusanya na kutupa  taka ngumu katika Halmashauri na Serikali za Mitaa  kote Nchini kuepuka kutupa taka kando ya Mito,Maeneo ya wazi,Barabara na katika Mitaro ya Maji.
Hayo yameelezwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.Angelina Mabula wakati akizungumza na wadau mbalimbali katika maadhimisho ya 33 ya siku ya makazi duniani ambayo hufanyika  jumatatu ya kwanza ya mwezi wa kumi kila mwaka.

Mabula amesisitiza kuwa kwa makampuni hayo kukusanya taka ngumu na kuzitupa ovyo si tu kuwa wanakiuka mikataba yao bali pia wanasababisha uharibifu wa mazingira,kuziba kwa mitaro na kuleta mafuriko.

Aidha pia Naibu Waziri Mabula ametoa wito kwa wananchi waishio mijini kuzingatia utaratibu uliowekwa wa kukusanya taka katika maeneo yaliyotengwa na kuchangia gharama  za kuondosha taka zilizowekwa ili waweze kuepuka namna ambayo inaweza kuathiri uharibifu wa mazingira.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi  Dolfin   yeye ametumia fursa hiyo kuelezea Historia ya siku hii ya Makazi Duniani.


Hatahivyo,Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya makazi Duniani kwa mwaka huu  inasema ‘’udhibiti wa taka ngumu mijini’’

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.