Header Ads

Katika kumuenzi Hayati baba wa taifa CCM wilaya ya ilala yafanya matembezi ya kilomita tatu


Chama cha Mapinduzi  Wilaya ya Ilala  katika kumuenzi hayati Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo  kimefanya  matembezi ya Kilomita tatu  yaliyoishia katika shule Sekondari Pugu.

Aidha wanachama hao wameshiriki zoezi la kufanya usafi katika shule hiyo na katika nyumba aliyoishi Mwalimu Nyerere kuanzi mwaka 1952 hadi 1955, akizungumza  katika shuguli hiyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma amewataka watanzania kumuenzi na kumuiga mwalimu Nyerere na kuyaishi maisha na matendo mema aliyoyatenda wakati wa uhai wake .


’’Watanzania tukimuiga  na kumuishi mwalimun  kama anavyofanya Rais wetu Dr John Pombe Magufuli nchi yetu itapigahatua kimaendeleo nawaomba watanzania na wanana ccm tumuenzi mwalimu kwa vitendo” alisema

Kwaupande wake  katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Joyce Ibrahimu Mkaugala,amasema  wanaIlala wamejitolea  katika matembezi na kufanya usafi katika juma zima na wameonyesgha moyo wa umoja katika kumuenzi Mwalimu haya yote nikunesha kuwa Mwalimu alikuwa ni kiangozi wa mfano.

“Mwalimu alitaka kila mtu awajibike afanye kazi  alikemea sana uvivi akiaminin kuwa kazi ndiyo njia pekee ambayo inaweza kuleta maendeleo pia alikemea ubaguzi wa rangi na ukabila na sisi hapa tuna sisitiza sote tuwe na ummoja”alisema

Naye mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Angelo Lwiza amewataka watanzania kumuenzi mwalimu Nyerere hasa katika nyumba alizoishi kuwekwevitabu alivyo vitunga na kuviandika mwalimu ili iwe kumbukumbu kwa vizazi vijavyo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.