Header Ads

Kocha wa klabu ya Tottenham Hortspurs, Mauricio Pochettino ameeleza kuwa klabu ya Espanyol ilikaribia kumnasa nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi mwaka 2005.Nyota wa Barcelona, Lionel Messi
Kocha wa klabu ya Tottenham Hortspurs, Mauricio Pochettino ameeleza kuwa klabu ya Espanyol ilikaribia kumnasa nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi mwaka 2005.
Amesema kuwa klabu ya Espanyol ilikaribia kumsajili nyota huyo alipokuwa mdogo katika kituo cha kukuzia vipaji cha Barcelona cha ' La Masia' mwaka 2005 wakati yeye akiwa katika hatua yake ya mwisho ya uchezaji wake katika klabu hiyo.
Akizungumza juu ya mchezaji huyo kuelekea mchezo wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Barcelona mjini London, Jumatano hii, Pochettino amesema,
"Nilianza kumsikia Messi tangu nikiwa Espanyol, akiwa ni kijana mdogo sana akicheza katika kituo cha La Masia. Alijiunga akiwa na miaka 13 kutokea Argentina hadi Barcelona na baadaye nikaskia kuwa Espanyol ilitaka kumsajili katika msimu ule ambao Barcelona ilicheza dhidi ya Juventus katika kombe la Joan Gamper ".
"Alicheza vizuri sana katika mchezo huo na kocha wa Juventus wakati huo, Fabio Capello alimsifia sana baada ya mchezo ndipo Barcelona walipobadili maamuzi ya kumuuza na kumbakiza katika kituo chao. Kwahiyo ukitazama katika historia hiyo,  asingecheza kwenye mashindano yale huenda leo tungemzungumzia ni mchezaji mkubwa Espanyol na Espanyol ingekuwa ni Barcelona ya sasa", ameongeza kocha huyo.
Messi alianza kuichezea Barcelona mwaka 2004 na ilikutana na Espanyol na kushinda kwa bao 1-0 katika Laliga.
Tottenham Hortspurs itakutana na Barcelona kwa mara ya kwanza katika michuano ya Ulaya tangu mwaka 1982, ambapo timu hizo zilikutana katika hatua ya nusu fainali ya kombe la washindi barani Ulaya na Barcelona kushinda kwa uwiano wa mabao 2-1

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.