Header Ads

Manchester City watateseka watakapotua kwenye Kona ya Anfield leo


Mwanamajinuni wa Anfield

Bill Shankly 1892

MLISEMA tuna ratiba ngumu lakini bado haijawa ngumu kwetu, hisabati ziko kama tulivyopanga.

Matokeo ya Napoli hayajanishtua, ni mjinga tu anaeweza kubeza ubora wao bila kujua Carlo Ancellot ana mataji matatu ya CL, na amecheza fainali mbili na mchezo wa makundi na sisi.

Anatufahamu..ingawa kilichotupeleka Italia ilikua ni point moja bahati mbaya tukaikosa dakika za mwishoni..

Je inatia wasiwasi?

Shaka hakuna hisabati ziko katika eneo letu bado, wengi wanasahau msimu uliopita tulipata matokeo ya ajabu ajabu sana kwenye makundi lakini tulicheza fainali.

Tulipata sare mbili na Sevilla, sare moja na CSKA Moscow na kuchukua alama sita kwa Maribor. Hatukua na kiwango cha kutisha kwenye hatua ya makundi.

Ndivyo tulivyoanza sisi, lazima ujue unataka nini katika kila mchezo, kuna mechi kocha anaamua kwenda kutafuta sare, zipo za ushindi pia.

Muhimu ni kujua tunacheza na nani, wapi na wakati gani. Bado nasisitiza hisabati ipo upande wetu wala hatuna wasiwasi.

Tuna point sita kwa Crvena Zvavda, tatu kwa Napoli Anfield na moja kwa PSG mnarani Ufaransa.

Maneno ni mengi kuwa hatuchezi vizuri...yeea inawezekana hatuchezi vizuri kwa uono wako, tuna point 19 sambamba na Man City kileleni mwa EPL unahitaji nini?

Tuna alama tatu kwenye kundi letu michuano ya UEFA, Napoli wana nne, PSG tatu na Red Star pointi moja. Unatubezaje? Mnatumia kipimo gani kutupima?

Wengine wamekuja na hoja kuwa washambuliji wetu wamekua butu, Sikiliza: Mane ana goli nne Ligi, Salah ana tatu na assist nne (kama sijakosea).

Hiyo 'flop' mnayoisema ni ipi?

Kwa miaka nenda rudi tumekua na tatizo zito la defense msimu huu tunaizungumzia Liverpool yenye ukuta mgumu kuliko hizo timu zenu zote za EPL.

Nazungumzia 'clean sheet' nne kwenye michezo saba ya Ligi ambazo nyanda wetu Allison Becker 'Pirlo' anazo mpaka sasa akikamata nafasi ya kwanza kwenye chati ya magolikipa ambao hawajaruhusu nyavu zao kuguswa kwenye Ligi.

Watu wanashindwa kuelewa katika Ligi isiyo na adabu kama ya England usipokua na nidhamu utaadhirika, mabingwa hucheza kwa heshima na tahadhari kubwa sana.

Hatutaki kufanya makosa kama yale ya Brendan Rodgers msimu wa 2013/14, lazima tuoneshe kuheshimu wapinzani wetu ingawa tunajua wana hofu kubwa na sisi.

Nimesikia kuna jamaa wa Chelsea anaongea kuhusu wao kututoa kwenye kombe la Carabao, nimjibu tu sisi tumechagua njia yetu wenyewe msimu huu.

Hatutaki ile ya pita huku na sisi tupite huku tukutane kwa mjomba, tumechagua kukaa njia kuu, tumekataa kuchepuka.

Tumetulia palipo na hitaji la mioyo yetu, hitaji la wanafamilia Milioni 70 wa Liverpool ulimwenguni kote. Ligi Kuu!

Kutolewa na Chelsea Carabao ni nafasi kubwa kwetu ya kupunguza ratiba na michezo mingi ambayo itatuchosha, tunahitaji timu iliyo imara na thabiti kumuezesha Jordan Henderson kunyanyua kwapa zake Mei 2019.

Siyo Carabao tu hata FA tutatolewa, ndoto ya waumini, wanazuoni, wanamajinuni na mashabiki wa Liverpool ni Ligi Kuu, hilo Carabao wapeni Watford.

Wakati huu ambao watoto wa Chelsea wanajivunia soka safi la SarriBalls walilokodishiwa na Gegen Pressing yake Klopp sisi tunawashukuru kwa ile Catenaccio yao walioachiwa na 'macho' Toni Conte.

Nini mnataka? Niandike kuhusu mchezo wa leo jioni dhidi ya Man City pale magetoni Anfield?

Haiwahusu hiyo tuachieni sisi muone tutawafanya nini, haya mtawafanya nini? Tutauchana mkeka wenu kisha tukae kileleni mwa Ligi.

Na tukirudi kwenye hisabati inaonesha Mkufunzi Jurgen Kaiser Klopp amekua na rekodi ya kibabe sana mbele ya tozi Pep Guaridola wa Manchester City.

Takwimu zinaonesha katika michezo 14 waliokutana Klopp ameshinda michezo saba, Guardiola akipata ushindi katika michezo mitano huku sare zikiwa mbili.

Takwimu zinaenda mbali zaidi zikimpa nafasi Klopp kwa kuonesha kuwa Klopp amekua na 51% za ushindi dhidi ya 35 za Guardiola lakini Kuli wetu wa Kijerumani akifunga magoli 22 dhidi ya 21 yake Guardiola.

Sasa kwa wale wanaojua maana ya namba wanaelewa jinsi gani City atadhalilika usiku wa leo mjini Merseyside. Kumbuka msimu uliopita Klopp alimchapa michezo mitatu Guardiola katika michezo minne waliyokutana.

Zaidi ya yote katika misimu minne ambayo Klopp amekua akihudunu Anfield hajapoteza mchezo hata mmoja dhidi ya Man City katika uwanja wetu wa nyumbani.

Unataka kula hela ya mchina, muhindi na mzungu kwenye mkeka wa mchezo huu? Usikae kiree wewe peleka mpunga kwa Liverpool wala usiangaike kuangalia Odds za mchezo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.