Header Ads

Mimi ni mbunge nina haki ya kufanya mikutano-BwegeMbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Seleman Bungara “Bwege” na wenzake wameachiwa kwa dhamana kufuatia kusambaa kwa taarifa za kukamatwa kwao na Jeshi la Polisi kwa madai kukiuka taratibu za ufanyaji wa mikutano ya hadhara kwenye Jimbo lake.
Akizungumza na www.eatv.tv Mbunge Bwege amesema yeye huwa haogopi kukamatwa na vyombo vya dola kwa kwa kile alichokidai ameshakamatwa mara kwa mara kabla ya kuwa mbunge.
Taratatibu zote mimi nilifuata na kila kitu nilipeleka polisi, mimi ni mbunge nina haki ya kufanya mikutano, lakini leo asubuhi wameniachia kwa dhamana, kesho tunafanya tena mkutano palepale nilipokamatwa jana mimi sihofii kukamatwa na kama nikiogopa basi niache tu ubunge, kukamatwa sijaanza leo nimekamatwa karibia mara 30 kabla sijawa mbunge.”, amesema Bwege.
Mapema jana kupitia mitandao ya kijamii kulisambaa taarifa ya kuwa mbunge huyo pamoja na na baadhi ya  viongozi wa Chama hicho kulisambaa taarifa ya kushikiriwa kwao na jeshi la polisi kwa kosa kufanya mikutano bila kufuata taratibu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.