Header Ads

Mkuu wa wilaya manyara ajipanda kutengeneza uwanja wa kwaraMkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti amejipanga kuhakikisha anautengeneza kisasa uwanja wa Kwaraa uliopo mjini Babati kwa kuuzungushia ukuta akishirikiana na wafanyabiashara waliopo ndani ya mkoa wake.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema alipokuwa akizungumza na mtandao huu kuhusu changamoto za Viwanja vya michezo katika mji wa Babati.

Fwema alisema Changamoto ya viwanja kwenye mji  wa Babati ipo kama zilivyo Halmashauri nyingine za miji,Manispaa na Majiji na maeneo mengine yanapopata sura ya Miji,lakini wamekuwa wakikabiliana nazo kutafuta ufumbuzi  wa muda mfupi na  wa kudumu ambapo wameanza kupima maeneo katika mashamba ya Katani kata ya Maisaka kwa ajili ya mipango ya muda mrefu.

Fwema amesema kwa sasa wanao mpango wa muda mfupi ambapo Halmashauri kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti waliwakutanisha wafanyabiashara  na kuzungumza nao kuhusu kuujenga  uwanja wa Kwaraa uliopo kati kati ya mji kwa kujenga vibanda vitakavyozunguka uwanja huo ambavyo vitakuwa vinafanana.

Amesema watamtumia mkandarasi kujenga vibanda hivyo vikubwa na vidogo na tayari menejimenti ya Halmashauri imeshaandaa michoro ambayo wataiwasilisha kwa kamati ya  mipango miji na kisha kwenye baraza la madiwani na baadae kuwaita wafanyabiashara wauone na wakishakubaliana waingie mkataba nao.

Fwema amesema watafungua akaunti inayojitegemea itakayokuwa ikitumiwa na Halmashauri na wafanyabiashara ambapo baada ya mkandarasi kumaliza ujenzi wataingia mkataba wa upangaji ambayo itazingatia gharama za kibanda ambacho mtu ameweka,kwamba afanye shughuli mpaka gharama yake irudi au awe anakata kidogo kidogo mpaka  gharama yake irudi.

Ameongeza kuwa pamoja na uwanja wa mpira utakaokuwepo lakini pia kutakuwa na viwanja vya michezo mingine ndani yake.

Mkurugenzi amesema vitu muhimu walivyokubaliana katika kikao walichoketi Halmashauri,mkuu wa Mkoa  na wafanyabiashara hao ni kuwapa kipaumbele zaidi wa nyumbani ndipo wafuate kutoka maeneo mengine ya Tanzania.

Amesema ipo mipango  ya muda mrefu waliyonayo ambapo  Halmashauri imeanza kupima maeneo mbalimbali yakiwemo ya Singu na Maisaka mashamba ya zamani ya katani na kote wamebainisha matumimizi mbalimbali ya ardhi ikiwa ni pamoja na  kiwanja kikubwa cha Michezo katika maeneo ya Katani na tayari wameshapeleka taarifa  Shirikisho la Soka Tanzania [TFF] waone ni namna gani watautengeneza uwanja huo.

Amesema kutokana na ukanda huu wa Bonde la Ufa unao vipaji vingi vya riadha TFF iliona itengeneze uwanja mkubwa wa kimataifa ili kuweza kuinua zaidi mchezo huo na michezo mingine Mkoani Manyara.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.