Header Ads

Mpango wa serikali juu ya wazee ni huuWAZIRI wa Fedha na Mipango Dk. Khalid Salum Mohammed amesema kuwa moja ya matunda ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kuwaenzi wazee kwa kuwapatia mahitaji muhimu yakiwemo makazi na afya bora.

Hayo ameyasema leo katika viwanja vya Bakharesa Fumba wakati wa hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wazee duniani.

Alisema kuwa suala la kuwaenzi wazee ni hatua moja wapo ya kujitathmini jitihada na mchango waliotoa katika harakati za Ukombozi wa taifa.

Alikumbusha kuwa Zanzibar inayo historia ndefu ya kuwaenzi, kuwatunza na kuwathamini wazee kwa kuwajengea makazi ya kudumu Unguja na Pemba pamoja kuwapatia huduma muhimu ikiwemo chakula, matibabu na posho la kujikimu maisha.

Waziri wa Fedha na Mipango  alisema kuanzia mwaka uliopita Serikali imeandaa utaratibu wa kuwapatia posho maalumu la kila mwezi wazee wote wenye umri wa kuanzia miaka 70 ili kuwapunguzia ugumu wa maisha.

Aliwataka Masheha kuhakikisha kuwa wazee wote wenye sifa waliomo kwenye maeneo yao wanasajiliwa kwa mujibu wa sheria ili kuweza kupata mahitaji yao wanayoyahitaji.

Alisema kuanzishwa siku ya wazee Duniani ni kutoa fursa kwa mataifa kutafakari changamaoto zinazowakabili wazee katika kuendesha maisha yao na kuzitafutia ufumbuzi wake.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.