Header Ads

Muuza gongo avua nguo ili asikamatwe


Katika Operesheni ya ukamataji wa pombe haramu aina ya Gongo

Operesheni iliofanyika Tarafa ya Mashati baada ya kupata Taarifa za Siri kuwa BI LEOKADIA (MAMA TINGISHA)
Amekuwa akiuza bangi na gongo kweye baa yake ya IMPALA wazi bila maficho kwa kuwa amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mmoja wa Askari wenye vyeo Tarafa ya Mashati ambae anamlinda (Jina limehifadhiwa)

Jambo ambalo lilisababisha Mhe DC Kujipanga na vyombo vya ulinzi na usalama kufanya upekuzi na kufanikiwa Kukamata Gongo na misokoto ya Bangi

Mtuhumiwa alitoa ushirikiano kwa kufungua vyumba vyote kwa upekuzi kasoro chumba kimoja ambacho alidai amempangisha mtu Mwezi mmoja na mhusika hayupo

Chumba hicho kilipofunguliwa ilikutwa Dumu la Pombe limeninginizwa kwa kamba nje ya dirisha likiwa na misokoto ya bangi

Baada ya Ugunduzi huo Mama Tingisha aliwatishia polisi kwa kuvua nguo zote na kubaki uchi wa unyama

Askari wa kike walitumia zaidi ya saa moja kumbembeleza avae nguo hadi walipotumia nguvu kumvisha nguo na kumpeleka kituo cha polisi.

Wananchi wa Mashati tunashukuru sana kwa tukio hili kwani huyu mama ameharibu sana watoto wetu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.