Header Ads

Mwili wa aliyefariki baada ya kuwekwa mahabusu azikwa


 Mwili wa Henry Kiwia, dereva wa daladala za Kiborlon aliyefariki dunia baada ya kuwekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Moshi umezikwa jana huku ndugu wakitaja mambo mawili wanayodai yana utata juu ya kifo cha ndugu yao.
Kaka mkubwa wa marehemu, Hudson Kiwia alieleza hayo jana katika kikao cha ukoo muda mfupi baada ya kutoka kuzika.
Akisoma taarifa ya uchunguzi wa kifo cha Henry kufuatia uchunguzi wa kifo chake uliofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC na daktari kutoka jijini Arusha, alisema ilibainika kuwa alinyongwa na kitu chenye mfano wa waya na alikutwa akiwa na nguo ambazo si zake.
Siku mbili zilizopita mwili huo ulichukuliwa na polisi na ndugu hao kutoka Hospitali ya Mawenzi na kupelekwa KCMC kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.