Header Ads

nampongeza sana amekuwa binti mkubwa mrembo na anafanya mambo mazuri-jideMsanii nguli kwenye game ya bongo fleva Judith Wambura marufu kama Comando Jide, ameweka wazi kuwa tayari kufanya collabo na msanii Caren, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mume wake mtangazaji Gardner Habash.

Akizungumza na mwandishi wa   www.eatv.tv  Jaydee amesema kwamba mikono yake iko wazi kumpokea binti huyo ambaye kwa sasa anakuja kwa kasi kwenye game ya bongo fleva, akiwa na kazi zake zinazoendelea kufanya vizuri.
Akimzungumzia Caren ambaye kwake alikuwa ni mama mlezi, amempongeza kwa kuwa binti mrembo na kuamua kuingia kwenye muziki rasmi, huku akimtaka kukaza buti.
“Kwanza nampongeza sana amekuwa binti mkubwa mrembo na anafanya mambo mazuri, kwa hiyo asikate tamaa kila kitu kinawezekana afuate ndoto zake ataweza kufanikiwa, kuhusu collabo anakaribishwa anytime mikono yangu iko wazi”, amesema Jaydee.
Hivi karibuni Caren alikuwa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kwamba kwenye game anamkubali Jaydee na diye mtu aligundua kipaji chake, wakati anaishi naye kama mama mlezi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.