Header Ads

Nataka mchumba wa kuinioa ndo mana nimetulia -pretty kind

STAA wa Filamu za Kibongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amedai kuwa amejifunza na hatarajii kurudi nchini India kujiuza kwani kwa sasa ametulia anachotaka ni kupata mchumba ili aolewe kwani maisha yamekuwa magumu.

 Pretty alifunguka hayo baada ya kuulizwa sababu ya utulivu wake wa hivi karibuni, huku wengi wakidhani amerejea kwenye biashara ya ukahaba nchini India ndipo aliposema kuwa kamwe hawezi kurudi nchini humo na maisha hayo ameshayasahau.

“Unajua watu wakiona umetulia watakusaka kwa lolote, mimi ninakua sasa mambo yote nimeacha ninachotaka sasa ni mchumba wa kunioa hivyo nimejituliza ili nione kama nitafanikiwa kwa hili kwani maisha ya sasa huwezi kupata mume bila kutulia,” alisema Pretty.
Mwaka juzi, Pretty alikiri kujiuza alipokuwa nchini India ambapo aliporejea nchini aliweka wazi kuwa anajutia jambo hilo na ameamua kuliacha kisha kujikita kwenye uigizaji na muziki.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.