Header Ads

Okwi awasha moto, Uganda yaikimbia TanzaniaTimu ya taifa ya soka ya Uganda 'The Cranes', imezidi kujiweka vizuri kwenye mbio za kufuzu fainali za AFCON 2019, baada ya jioni hii kushinda mechi yake katika Kundi L dhidi ya Lesotho na kufikisha alama 7 kileleni.
Uganda imeshinda mechi hiyo ambayo ni ya tatu kwenye kundi hilo kwa jumla ya mabao 3-0. Nyota wa Simba Emmanuel Okwi amehusika katika mabao yote kwa kufunga mawili na kusababisha penati ambayo ilizaa bao.
Mabao mawili ya Okwi ameyafunga katika dakika za 12 na 64 ya mchezo huku Farouk Miya akifunga kwa penati katika dakika ya 37.
Uganda ambayo ipo kundi 1 na Tanzania sasa imeshinda mechi 2 na kutoa sare 1 dhidi ya Tanzania. Cape Verde ambao wameshinda mechi moja na kutoa sare moja wakipoteza moja wapo katika nafasi ya pili wakiwa na alama 4.
Tanzania imeendelea kushika mkia katika kundi hilo baada ya jana kukubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Cape Verde, hivyo kubaki na alama 2 sawa na Lesotho ambao wapo katika nafasi ya 3.
Jumanne ya Oktoba 16, 2018 Tanzania itaikaribisha Cape Verde kwenye dimba la taifa jijini Dar es salaam. Mchezo huo utakuwa ni wa 4 kwa Tanzania katika kundi L, ambapo itahitaji kushinda ili kufufua matumaini ya kufuzu fainali hizo zitakazofanyika nchini Cameroon.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.