Header Ads

RC aagiza Mwenyekiti wa wilaya CCM akamatwe


Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti ameagiza kukamatwa kwa mwenyeikiti wa Chama cha mapinduzi wilaya ya simanjiro kufuatia tuhuma za uchochezi wa migogoro ya ardhi ikiwemo mgogoro wa kugombea kitongoji cha katikati baina ya vijiji vya kitiiengare na sukuro kata ya Komolo.

Maagizo hayo ya mkuu wa mkoa wa manyara anayatoa siku chache baada ya mwenyekiti huyo kufanya mkutano na wananchi kwenye kijiji cha kitiiengare mkutano ambao unaelezwa kuwa ni wa kiuchochezi juu ya mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka kumi kwa mujibu ya wananchi wenyeji na kupelekea kukwamisha maendeleo ndani ya vijiji vyote viwili huku pia mwenyekiti huyo pamoja na kamati yake ya siasa chama cha mapinduzi wakishutumiwa kuitukana serikali mara kadhaa kwenye mikutano yao.

Ikafuata onyo kwa wanasiasa wote ndani ya simanjiro na mkoa wa Manyara kwa ujumla ambao wamekuwa wakifanya siasa za kuchochea migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi na kutumia matatizo ya wananchi kuwa fursa ya kujijengea umaarufu kisiasa.

Mwenyekiti huyo Awadhi Omary akazungumza kwa njia ya simu juu ya mgogoro huo anaohusishwa.

Nao wananchi wakatoa yamoyoni juu ya mgogoro huo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.