Header Ads

Wakulima wa korosho wapewa somoMKUU wa wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi,Christopher Ngubiagai amewaasa wakulima wa korosho wasibweteke na kujiona kwamba niwao tu wanaolima zao hilo hivyo kushindwa kuandaa mazingira mazuri ya ushindani.

Ngubiagai alitoa angalizo hilo wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wajumbe wa bodi,viongozi na watendaji wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) vilivyopo wilayani humo. Mafunzo yaliyoandaliwa na idara ya ushirika ambayo yalifanyika katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko.

Ameongeza kuwa ingawa tahadhari hiyo inalenga wakulima wa wilaya ya Kilwa, lakini inaweza kuwanufaisha wakulima wa zao hilo nchini. Kwa kuzingatia historia ya zao hilo nchini hwana sababu ya kubweteka nakushindwa kuchukua tahadhari ili waweze kukabiliana na ushindani katika uzalishaji na ubora wa zao hilo.

Alirejea kuwakumbusha historia ya zao hilo kwa kusema mwanzo lilizalishwa na mikoa mitano tu hapa nchini.Lakini hadi sasa mikoa 17 inalima.Huku nchi nyingi zikianza kulima.Hali ambayo itasababisha ushindani nje na ndani ya nchi.

"Nchi yetu ni yanne kwa uzalisha korosho duniani.Kwahapa nchini mikoa ya Lindi na Mtwara ndiyo inabeba nchi kwa uzalishaji mkubwa.Hata hivyo nchi ya Zambia imeanza kulima,China muda si mrefu asilimia  thelathini ya mahitaji yake itaptikana kutoka kwa wakulima wake,"alisema Ngubiagai.

Kufuatia hali hiyo aliwaasa wakulima kuhakikisha ubora wa zao hilo unakuwa kwenye kiwango kinachoweza kuhimili ushindani wa soko la ndani na nje ya nje.Huku akionya wasibweteke nakujiona wamehodhi uwezo wakuzalisha zao hilo peke yao.

Aidha mkuu huyo wa wilaya ya Kilwa alitoa wito kwa viongozi na watendaji hao wa AMCOS  wajipange kuanzisha viwanda vidogo ili kuongeza thamani ya zao hilo,ili kwenda na dhamira ya serikali ya uchumi wa kati kupitia viwanda.

Alisema AMCOS zikisindikiza korosho na matunda yake(mabibo)  zinaweza kupata fedha nyingi.Huku akiweka wazi kwamba matunda ya korosho yakitengenezwa vinywaji yatakuwa na bei kubwa kuliko korosho zenyewe.

"Mabibo yanayoweza kutoa kilo moja ya korosho yanaweza kutengeneza waini(wine) yenye thamani ya shilingi 70,000.Yakitengenezwa jamu kwa ajili ya mikate itauzwa shilingi 28,000.Wakati korosho ghafi zinauzwa kwa shilingi 4,000 tu," alisisitiza Ngubiagai.

Katika kuhakikisha anapita nakutembea juu ya maneno yake  Ngubiagai amewaonya viongozi na watendaji hao wahakikishe wanakagua vizuri ubora wa korosho.Kwani serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi na watendaji ambao vyama vyao vitabainika kuingiza sokoni korosho chafu.

Ngubiagai aliwaonya pia wanunuzi wanaonunua zao hilo kinyume cha taratibu na sheria(walanguzi) kwamba serikali wilayani humo imejipanga vema kuthibiti vitendo hivyo na hujuma zote dhidi ya ubora wa zao hilo.

Alifafanua kwamba walanguzi licha ya kuwadhulumu wakulima,lakini pia wanachangia kuingizwa korosho chafu kwenye vyama vya msingi na hata kwenye maghala yanayokusanyiwa korosho kutoka kwenye vyama vya msingi.Huku akiweka wazi baadhi ya korosho hizo zinatoka nje ya wilaya hiyo na mkoa huu wa Lindi.

Kwaupande wao viongozi na watendaji hao wa AMCOS waliiomba serikali ihakikishe  viwatilifu vipatakena muda wote kama bidhaa nyingine.Badala yakupatika wakati wa msimu pekee kama ilivyo sasa

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.