Header Ads

Wananchi wajitokeza kupiga kura

 Wananchi mbalimbali wamejitokeza katika kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Jang'ombe.

Akizungumza na waandishi wa Habari mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama mkoa wa Mjini magharib Unguja Mhe,Ayoub Mohammed Mahmoud amesema hali ya Ulinzi na Usalama imeimarika katika eneo lote la Jang'ombe.

 "Hadi sasa tunashukuru hali ya ulinzi na usalama ndani ya Jimbo na mkoa mzima tumeimarisha alisema RC Ayoub.

Aidha Ayoub amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi na kupiga kura kwa amani na utulivu.
Hata hivyo amesema hali ya Demokrasia Zanzibar imeimarika kwani amefarijika kuwaona mawakala takribani wote 8 wa vyama vyote wamekaa katika benchi moja na hakuna malalamiko yoyote.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.