Header Ads

WATANZANIA WASHAURIWA KUUENZI UTAMADUNI WAOWAZIRI MKUU wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh  Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuuheshimu na kuuendeleza utamaduni ambao ndio urithi wao ili kulifanya Taifa liendelee kuwa hai.

Ameyasema hayo oct 26 mwaka huu alipotembelea shughuli za Tamasha la utamadini wa Mtanzania kwa jamii ya watu wa Lindi ambapo amesema kuwa suala la kuuenzi utamadini ni jambo zuri ambalo linatoa fursa kwa watu wengine hususan wa mataifa ya nje kuja kujifunza historia ya Watanzania na maisha yao.

Aidha, Katika tamasha hilo linalofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alitumia nafasi hiyo kuwataka Watanzania waendelee kuupenda utamaduni wao.

kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi amesema mkoa umetumia tamasha hilo kutoa ujumbe kwa umma kuhusu vivutio mbalimbali walivyonavyo pamoja na fursa za uwekezaji.
Hatahivyo,Waziri Mkuu amesema tamasha limewakutanisha Wanalindi kutoka katika wilaya mbalimbali linatoa fursa ya wao kujadili maendeleo ya mkoa wao na Taifa kwa ujumla. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.