Header Ads

Anacho kifanya zari si cha kitoto ni mambo makubwa

Zari ni Habari  Nyingine Ulinzi Wake si wa Nchi Hii
ACHANA na dili alizolamba kupitia makampuni mbalimbali kipindi akiwa na mzazi mweziye ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kabla ya kuachana kwao Februari, mwaka huu.  Mwanamama mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ mbali na kupata dili hizo kwa sasa amezidi kuonesha kuwa kweli ni Zari The Bosslady baada ya kupata ulinzi kila kona alipotua ndani ya Jiji la Kampala.

Zari yupo nchini humo baada ya kupata shavu kutoka Wizara ya Utalii kuwa balozi wa utalii atakayokuwa akitangaza utalii nje ya Uganda. Mwanamama huyo ambaye yupo sambamba na Waziri wa Utalii nchini humo, Godfrey Kiwanda amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki mbalimbali baada ya kutembelea mitaa mbalimbali eneo la Mbarara.

Kupitia kampeni yake ya kuhamasisha utalii aliyoipa jina la Tulambule Ne Zari (Tutembee na Zari) aliongozana pia na mabodigadi waliokuwa na sare pamoja na silaha kali.

Timu hiyo iliyokuwa na msafara kama wa rais ambapo gari ya kifahari maalumu kumbeba Zari aina ya Toyota Land Cruiser V8 iliandikwa jina lake na kutua katika sanamu ya Uhuru kisha Equator na kumalizia Soko la Lukaya.

Kwa sasa, Zari anatajwa kama mmoja wa mastaa wakubwa nchini Uganda akipewa kipindi maalum cha TV ambacho lengo lake kuwavutia mashabiki wake wengi kuingia nchini Uganda.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.