Header Ads

Dkt. Kilahama awauma sikio watu wa Lindi, awaonesha dili

WAHENGA walipata kusema,aliyeandikiwa kupata atapata tu.Ndivyo inavyoonesha kutimia ukweli wa msemo huo kwa watu wa mkoa Lindi.Nikufuatia habari njema iliyoelezwa na mwenyekiti wa bodi ya shirika la uhifadhi na uendelezaji mpingo(MCDI),Dkt Felician Kilahama.

Dkt Kilahama ambae aliwahi kuwa mkurugenzi wa idara ya misitu na nyuki iliyokuwa chini ya wizara ya maliasili na utalii,amewaasa wananchi wa mkoa huu wa Lindi walinde na watunze kwa nguvu zote mianzi miti.Kwani nibiashara mzuri inayolipa.

Dkt Kilahama ameyasema hayo kwenye warsha ya wadau wa misitu ambayo imeanza leo katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko.Warsha ambayo imeandaliwa kwa ushirikiano wa shirika la uhifadhi na maendeleo ya Mpingo(MCDI),Shirika la kimataifa la uhifadhi wa mazingira(WWF)na halmashauri ya wilaya ya Kilwa.

Dkt Kilahama alisema wananchi wa mkoa wa Lindi wanabahati kuwa na mianzi miti ambayo inatumika kutengeneza bidhaa za aina nyingi.Hivyo wanakila sababu ya kulinda na kuhifadhi miti hiyo ambayo alisema inapatikana kwa wingi mkoani humu.

Katika kuthibitisha mianzi hiyo nibiashara itakayokuwa na soko kipindi kifupi kijacho,Dkt Kilahama alisema MCDI imeanza kufanya maandalizi ya kimkakati juu ya miti hiyo.Kwani katika mkoa huu inapatikana kwa wingi na katika eneo kubwa.

"Mkakati wetu wa kwanza nikutengeneza baiskeli kwa kutumia mianzi miti.Niimara inayofaa kutengenezea baiskeli na bidhaa nyingine nyingi.Kwahiyo watu wasiruhusu kukatwa ovyo,"alisisitiza Dkt Kilahama.

Kilahama huku akionesha kujiamini kuhusu uhakika wa soko la maliasili hiyo,alisema shirika hilo lingependa kuona miti hiyo inakuwa miongoni mwa vichocheo vya uchangiaji uchumi na maendeleo ya wananchi wa mkoa huu na taifa.

Mbali na kuwapa habari hiyo njema wananchi wa mkoa wa Lindi,hasa wanaoishi kwenye maeneo yanayopatikana miti hiyo.Mwenyekiti huyo wa bodi alizipongeza wilaya za Rufiji,Kilwa,Namtumbo na Tunduru kwa jitihada kubwa za kusimamia na kutunza misitu.Jitihada ambazo zimeanza kuzaa matunda kwani wananchi wameanza kunufaika kupitia misitu.

Kwa upande wake meneja uhifadhi wa shirika la kimataifa la kuhifadhi mazingira(WWF),Dkt Simon Lugandu alisema shirika hilo lipo bega kwa bega na wananchi katika suala zima la ulinzi wa raslimali na maliasili.Ikiwemo ulinzi wa wanyama pori,viumbe vya baharini,misitu na mazingira.

Alisema ingawa uchumi wa nchi yetu unategemea maliasili tulizonazo kwa ajili ya ustawi wa wananchi na taifa.Lakini kunatishio kubwa kuhusu usalama wa maliasili hizo.Kwani kunauharamia baharini,uvuvi haramu,uchomaji na ukataji ovyo misitu,uwindaji haramu wa wanyama pori(ujangili) na mengine mengi yanayosababisha baianuai kupungua.

Warsha ya wadau wa misitu ya mwaka huu ni yakumi kufanyika tangu kuanza kufanyika mwaka 2007.Ambapo hufanyika kila mwaka.Ikielezwa kwamba warsha ya mwaka huu ambayo itafanyika kwa muda wa siku tatu inawashiriki takribani 200.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.