Header Ads

Ghorofa la Harmonize Lazua Gumzo

Ghorofa la Harmonize Lazua Gumzo
Msanii wa muziki Harmonize ameacha maneno midomoni mwa watu baada ya mwana muziki huyo  kuonekna akiwa katika moja ya hatua za ujezi wa nyumba yake kubwa lililopo maeneno ya tandale.

Jumba hilo ambalo ni ghorofa limeonekna bado katika kumalizia lakini kwa wale walioliona na kulithaminisha wanasema kuwa nyumba hiyo itakuwa kubwa sana kiasi kwamba litakapo isha litakuwa na kufuru kubwa.

Harmonize nae amekuwa akifanya mambo mengi yenye kuonyesha mafanikio yake huku akiwakumbuka hata watu wa nyumbani kwao kwa kuwajengea msikiti kwa udhamini wa bosi wake.

Watu wa karibu na ulipo mjengo huo walikiri kuwa mjengo huo mkubwa ni wa mwanamuziki Harmonize kwa sababu mara nyingi wamekuwa wakimuna mama wa msanii huyo akija kuongea na kusimamaia mafundi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.