Header Ads

Hali ya hawa yaendelea kuimarika

Babu Tale Afunguka Kuhusu Afya ya Hawa "Anaendelea Vizuri na Yuko Tayari Kurudi Nchini"
Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale ametoa taarifa kuwa msanii wa muziki nchini Hawa Said maarufu kama Hawa wa Diamond anaendelea vizuri .Ikumbukwe Hawa alikuwa na tatizo la ini ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini na Babu Tale ndio alipewa jukumu la kusimamia matibabu yake nchini India kwa kuwa gharama zote za matibabu alizitoa Diamond Platnumz.

Ujumbe wa Babu Tale ni huu hapa:-Asante Mungu, asanteni watanzania kwa dua zenu. Hawa sasa yupo salama kabisa... Ameshatoa nyuzi na yupo tayari kurudi nyumbani. Haikua kazi rahisi kupitia alipo pitia, pia tunaomba muendelee kutuombea dua ili tuwe na nguvu ya kuendelea kusaidia wenzetu. Haikua rahisi kumuacha mgonjwa siku ya kwanza anatoka theatre, ila ilibidi nirudi kusimamia majukumu mengine... nikikumbuka alivyonililia mama yake mpaka nikatamani nisirudi TZ, ila majukumu mengine yalifanya nirudi. Amka uende kusali, Mungu yupo na dua pia zipo!!! maana kila nikikumbuka lile tumbo la Hawa, na Leo halipo tena... maana yake Mungu alikua anataka kuonyesha nguvu zake!! Nakumbuka aliniambia lile tumbo amekaa nalo mwaka mmoja na nusu, ila kwa nguvu ya Mungu limeondoka ndani ya mwezi mmoja, SubhanaAllah!! anasema anajiona mwembamba na mwili hajauzoea... Ijumaa Kareem

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.