Header Ads

Hatimaye Mama Mercy Anna Mengi Azikwa Moshi

Hatimaye Mama Mercy Anna Mengi Azikwa Moshi
Mwili wa mmoja wa waanzilishi wa makampuni ya IPP Mama Mercy Anna Mengi, umezikwa leo eneo la Wari Machame Moshi, Mkoani Kilimanjaro ambapo mamia ya watu kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Kilimanjaro na Dar es salaam wameshiriki mazishi hayo.

Awali mwili wa Mama Mercy Anna Mengi uliagwa katika Kanisa la KKKT usharika wa Moshi mjini, ibada ambayo iliongozwa na Askofu Dkt Fredrick Shoo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na watu maarufu.

Katika ibada hiyo pia Makamu wa Rais, Samia Suluhu pia alishiriki ambaye aliambatana na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jaffo pamoja na viongozi wengine wa kisiasa akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe.

Mama Mercy Anna Mengi aliaga dunia tarehe 31 Oktoba, 2018 katika hospitali ya Mediclinic Morningside, Johannesburg Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wa Marehemu Mama Mercy Anna Mengi uliwasili Jijini Dar es Salaam tarehe 7 Novemba, 2018. Na Ibada ya kumuaga ilifanyika katika Kanisa la Azania Front Alhamis ya tarehe 8 Novemba 2018 jijini Dar es salaam.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.
Amen.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.