Header Ads

Himid Mao ,Abdi Banda timu zao ziko katika hali mbayaWALINZI wawili tegemeo wa Taifa Stars, Himid Mao na Abdi Banda timu zao ziko kwenye hali mbaya kwenye Ligi. Banda ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba, anaichezea Baroka ya Afrika Kusini na Himid anakipiga Petrojet ya Misri.

Katika misimamo ya Ligi zao, timu zote zipo kwenye nafasi ya pili kutoka mkiani. Baroka ina pointi 7 ikiwa imecheza mechi Banda, Himid hali tete klabuni kwao 11, huku Petrojet ikiwa nazo 10 katika michezo 12.

Uongozi wa Baroka umeweka wazi hivikaribuni kwamba hauna mpango wa kubadilisha tena kocha kwa madai kwamba ndio sababu ya timu hiyo kuyumba kwenye miaka ya hivikaribuni.

Petrojet inamilikiwa kampuni ya mafuta ya Petrojet yenye maskani yake maeneo ya Suez, wako kwenye mkakati wa kubadilisha mambo mengi katika kikosi hicho na kuirudisha timu hiyo kwenye ubora wake wa zamani.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.