Header Ads

Idadi ya watoto wanaozaliwa imepungua


Watafiti wanadai kwamba idadi ya watoto ambao wanazaliwa imepungua duniani kote kwa kiwango kikubwa.
Utafiti huo umebainisha kwamba idadi ya watoto wanaozaliwa imeshuka na wengine hushindwa kuzaliwa baada ya kuharibika.
Watafiti wamedai kwamba matokeo ya utafiti huo uliwashangaza sana.
Na hali hii imepelekea kwa jamii kuwa na wazee wengi zaidi ya wajukuu.

Ni kwa kiasi gani idadi ya wanaozaliwa imepungua?

Utafiti ambao ulichapishwa huko Lancet, ulifuata mwenendo wa kila nchi kuanzia mwaka 1950 mpaka 2017.
Mnamo mwaka 1950, wanawake walikuwa na watoto takribani watano. Na kiwango cha kujifungua kwa kila mwanamke ilikuwa ni watoto wawili kwa mwaka jana.
Lakini hali hiyo ina utofauti mkubwa kati ya nchi na nchi.
Kiwango cha watoto wanaozaliwa nchini Niger ni watoto saba wakati kwenye fukwe za bahari ya Mediterania, wastani wa mwanamke kujifungua ni mtoto mmoja.

Je, ni kwa kiasi gani idadi ya wanaozaliwa inabidi iwe?

Kipindi ambacho idadi ya watoto wanaozaliwa inapungua kwa wastani wa watoto wawili basi idadi ya watu pia itaathirika.
Takwimu ya watoto wanaoharibika pamoja vifo vya watoto wachanga vimeongezeka.
Mwanzoni mwa utafiti huo mnamo mwaka 1950,hakukuwa na taifa hata moja ambalo lilikumbana na changamoto ya kupungua kwa idadi ya watu wanaozaliwa.
Profesa Christopher Murray,mkurugenzi wa chuo kikuu cha afya na tathmini kilichopo mjini Washington aliiambia BBC kuwa " tumefikia mahali ambapo nusu ya mataifa yana upungufu wa watoto wanaozaliwa dhidi ya waliopo".
Hivyo kama hakuna hatua ambayo itachukuliwa basi idadi ya watu itapungua katika hayo mataifa".
Aliongeza kwa kudai kwamba mabadiliko haya yamewashangaza wengi .
"Idadi ya watoto wanaozaliwa imepungua nusu ya mataifa yote duniani, kiwango hicho ni kikubwa na kinastaajabisha" Prof.Murray alieleza.

Ni mataifa gani yameathirika?

Nchi ambazo zimeendelea zaidi kiuchumi zikiwemo nchi zilizopo barani ulaya,Marekani,Korea Kusini na Australia kuna kiwango kidogo cha watoto ambao wanazaliwa.
Aidha hii haimaanishi kwamba idadi ya watu wanaoishi katika mataifa hayo imepungua.
Kwa sasa bado kiwango cha idadi ya watu imechanganyika na wanaozaliwa na kufa pamoja na wahamiaji.
Hii inaweza kubadili kiwango cha wanaozaliwa
Lakini Profesa Murray anasema kwamba hali hii inapelekea dunia kufikia hatua ambayo jamii itaanza kuathirika kwa kupungua kwa idadi ya watu.
Nusu ya mataifa dunia bado wanawake wanazaa watoto wanaotosha lakini kadri nchi zinavyodhiki kukua kiuchumi ,idadi ya wanaozaliwa pia inapungua.

Kwa nini idadi ya wanaozaliwa inaoungua?

Kupungua kwa kiwango cha watoto wanaozaliwa haitokani na watu kushindwa kuwa na nguvu ya kuzaa au jambo lolote linalohusisha na uzazi.
Aidha kuna mambo makuu matatu ambayo yanasababisha;

Bila ya kuwa na uhamiaji, mataifa yataangaika na suala la umri na kupungua kwa kiwango cha watu.
Dr George Leeson, Mkurugenzi wa chuo cha Oxford anasema kwamba hali hiyo sio jambo baya ilimradi jamii yote aiathiriki na kiwango cha mabadiliko hayo kwa kiasi kikubwa.
Ameiambia BBC, kiwango hicho kimeathiri maisha ya kila mmoja.
Ukiangalia watu mitaani , kwenye makazi yao na foleni za barabarani .
Matumizi yao yanategemea kiwango cha watu kilichopo.
Kila kitu ambacho tunapanga kinatokana na idadi ya kiwango cha watu lakini vilevile vile ,umri wao pia huwa unaleta mabadiliko.
Mtaalam huyo anafikiri kwamba maeneo ya kazi yanaweza kubadilika na hata kuwataka watu wastaafu kufanya kazi wakiwa juu ya umri wa miaka 68 ambao ndio kiwango cha mwisho nchini Uingereza.
Nchi ambazo zimeathirika zitahitajika kuongeza idadi ya wahamiaji na kuanzisha sera mpya ili kuwahamasisha wanawake kuzaa watoto zaidi ambapo mara nyingi inashindikana.
Muandishi wa ripoti hiyo Profesa Murray amebaini kwamba kutakuwa na watoto wachache na watu wengi ambao wana umri juu ya 65 hivyo itawawia vigumu kukabiliana na mabadiliko haya duniani.
Ukifikiria juu ya matokeo ya kiuchumi na kijamii ya namna ambavyo kuna bibi na babu wengi zaidi ya wajukuu.
Nadhani Japan inafahamu kuwa ina upungufu wa idadi kubwa ya kiwango cha watu wanaozaliwa.
Lakini nchi nyingi zilizopo kaskazini hazitaathirika kwa sababu ya idadi ya watu waliopungua itafidiwa na wahamiaji.
Ingawa kiwango cha watu duniani, hakuna suluhisho la uhamiaji.
Mabadiliko hayo yanaweza kuathiri jamii, vilevile kutakuwa na mafanikio ya kimazingira ambayo yataleta manufaa katika jamii yetu.

Vipi kuhusu China?

China ina kiwango kikubwa cha ongezeko la watu tangu mwaka 1950, ambapo inakadiriwa kuwa nusu bilioni ya kiwango cha watu wote.
Lakini bado wanakumbana na changamoto ya kiwango cha watu wanaozaliwa ambayo inafika 1.5 kwa mwaka 2017 na kuwapelekea kwenye sera ya kuwa na mtoto mmoja tu.
Sababu za nchi zinazoendelea kuhitaji kuongeza idadi ya watu wanaozaliwa cha 2.1 ni kwa sababu sio watoto wote huwa wanaweza kuishi ya kufikia utu wazima na watoto wengi ni wavulana zaidi ya wasichana.
Nchini China, Utafiti unaonyesha kuwa kila watoto 100 wanaozaliwa , kuna watoto 117 wakiume wanazaliwa.
Watoto wengi wanahitajika kuzaliwa ili kuwe na idadi imara ya kiwango cha watu.
Chanzo BBc

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.