Header Ads

JAFO APONGWEZA NA WANAFUNZI WANAOISHI KTK MAZINGIRA MAGUMUWANAFUNZI wa shule za msingi wanaoishi katika mazingira magumu wilayani Kongwa wamewaomba viongozi wa serikali wakiwemo mawaziri,na wabunge kuiga mfano wa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (TAMISEMI) Seleman Jaffo ambaye ameweza kuwasaidia vifaa mbalimbali vya elimu.
Shukrani hizo zimetolewa baada ya kukabidhiwa madaftari 4,080 yaliyotolewa na waziri huyo kwa kushirikiana na wadau wa elimu kwenye shule tano za msingi zilizopo katika kata ya Sejeli wilaya ya Kongwa mkoa wa Dodoma.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi wa shule ya msingi Mbande Helman Robert na Theobal Augustino wote wa darasa la nne,walisema kitendo kilichofanywa na Waziri Jaffo kwa kushirikiana na wadau wa elimu kitawawezesha kufanya vizuri kwenye masomo yao.
“Ukizingatia sisi ni wanafunzi tunaotoka kwenye familia masikini,ambao tulio wengi uwezo wa kununua vifaa vya elimu ni mdogo,hivyo kwa kitendo hiki tunaishukuru serikali kwa kupitia waziri Jaffo na washirika wezake ambao wametusaidiA haya madaftari na tunamwakikishia tutafanya vizuri kwenye masomo yetu”alisema. Augustino.
Awali akikabidhi msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kongwa Dkt Omary Nkullo kwa kushirikiana na mwakilishi wa wadau wa elimu Keneth Yindi,aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha wanatumia fursa hiyo ya kusaidiwa kumuunga mkono Rais ambaye hivi sasa amewaondolea michango mbalimbali ikiwemo ada.
Dkt Nkullo aliwataka wanafunzi pia kutokatishwa na tamaa pale wanapoona wamesaulika katika kuwapatia misaada bali serikali kwa kushirikiana na wapenda elimu wataendelea kutoa misaada ili na wao waweze kufanya vizuri kwenye masomo yao.
“Sasa tazameni leo hii mmepata madaftali ya kutosha yaliyotolewa na waziri wenu kwa kushirikiana na wadau wa elimu,na mimi naamini mtapewa zaidi ya haya,ila kinachohitajika ni kujibidisha kwenye masomo yaenu na msiwaangushe hawa wadau wanaowasaidia”alisema.
Kwa upande wake mwakilishi wa wadau wa elimu Keneth Yindi aliwataka wazazi wenye watoto wanaoishi katika mazingira magumu kutoutumia msaada huo kinyume na malengo yaliyokusudiwa,bali yatumike kwa ajili ya kuandikia wanafunzi hao.
“Itasikitisha sana kwa waziri wetu pamoja na washiriki waliochangia madaftali hayo kuona wazazi mnauza na hamtoi msaada hata wa kufuatilia kama mtoto anayatumia kwa malengo husika hii itatusikitisha mno”alisema.
Mwakilishi huyo ambaye pia ni Diwani wa kata ya Buigiri katika Halmashauri ya Chamwino aidha aliwataka wazazi kutowashawishi wanafunzi kufanya vibaya kwenye masomo kwa malengo wasije wakafaulu ili waweze kuridhi mifugo na wengine kutakiwa kuolewa na kuoa.
“Kitendo hicho kinaweza kuwakosesha Taifa kuwapata viongozi,leo unamfundisha afanye vibaya kwenye masomo yake,je viongozi wasomi watatoka wapi na kama siyo hao ambao mnawafundisha wafanye vibaya kwenye masomo hayo ninawaomba wazazi wengu tuondokane na tabia hiyo”alisema.
Naye Diwani wa kata hiyo Chilingo Chimeledya alisema pamoja na msaada uliotolewa na waziri huyo na wadau wa elimu pia baadhi ya viongozi wakiwemo wa chama na serikali wamemuunga mkono Rais kwa kuweza kutoa vifaa hivyo vya elimu kwa wanafunzi hao.
Chimeledya alitaja viongozi ambao walioweza kuunga juhudi hizo ni pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo aliyetoa daftali 334,madiwani wote wa halmashauri  bosk moja kila mmoja,mwenyekiti wa halmashauri boksi mbili,mwenyekiti wa huduma ya jamii boksi mbili,mwenyekiti wa kijiji daftali 100.
Diwani huyo ambaye katika kata yake jumla ya shule tano ikiwemo ya Sejeli,Manungu,Mbande,Mlimagati na Msujilile zilipatiwa msaada huo wa madaftali  alitaja Wengine ambao wameunga juhudi hizo za Rais ya kuifanya elimu hiyo kuwa bure katika serikali ya awamu ya tano ni pamoja na serikali ya kijiji ambayo imeahadi daftali 100.
MWISHO.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.