Header Ads

Jambo hili ni muhimu ili kuleta ushindani katika biashara unayoifanya.

Miongoni mwa mambo yatakayokusaidia kuweza kusonga mbele husasani katika kipengele cha biashara ni kuweza kuwa bora katika biashara ambayo unaifanya.

kama leo ukienda sokoni kuna bidhaa na huduma nyingi ambazo ni za aina moja, lakini siyo zote zinafanya vizuri unajua hii inatoakana na nini, Hii ni kutokana na baadhi ya bidhaa au huduma kutozingatia kuwa na tija kwa wateja wake. Ikiwa unatengeneza bidhaa au huduma fulani hakikisha itakuwa na manufaa makubwa na ya uhakika kwa wateja wako.

Kwa mfano nimewahi kuona vitafunwa vilivyoandaliwa katika mazingira duni na kuwa na dosari mbalimbali kama vile marashi, vipande vya nywele, mchanga n.k. Ni wazi kuwa bidhaa za namna hii zitakosa wateja kutokana na kuwa na ubora duni.

Kila mara kumbuka kuwa ushindani ni mkubwa, hivyo jitahidi kuongeza tija na ubora wa huduma na bidhaa zako. Pia usipende kufanya kile kitu ilimradi unafanya tu bali unatakiwa kujiuliza hivi ni kwa kwanini wateja wanakuja kwangu na hawaendi sehemu nyingine?
Mpaka kufika hapo hatuna la ziada, endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.