Header Ads

Konkoi Konki konki Master inavyo shangaza wengi

Kwa sasa msanii Dudu Baya ameviteka vyombo vya habari kwa upande wa Burudani na mitandao, kila kona ni Konkoi Konki konki Master. Tunaweza kusema ni ubunifu wake au ni kipindi ambacho upepo wa yeye kujadiliwa (trend) umempuliza.

Hapo juzi November 07, 2018 Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aliyejkulikana kwenye muziki kama MR II 'sUGU' alipata nafasi ya kuimba mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Dodoma.

Wakati MC wa tukio hilo anamkaribisha Sugu alitamka maneno 'Konkoi konki konki Master' Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani msempo huo kwa sasa umekuwa maarufu hadi mbele ya waheshimiwa umeweza kutambulika. Msemo huo hadi sasa una maana tatu kwa Dudu Baya.

1. Ukitoa wasanii wa WCB, Dudu Baya ni msanii wa kwanza kabisa kuhakikishiwa kuwa atakuwepo kwenye tamasha la Wasafi Festival. Hii ni kutokana na kuanza kutikisa kupitia 'Konkoi konki konki Master'.

Kubwa zaidi ni kuwa msemo wake huo umeingia kwenye slogan ya tamasha hilo, hakuna aliyetarajia hilo kwani Dudu Baya ni msanii ambaye hakuwa kwenye chati kabisa za kimuziki na sio mtu wa kufanya matangazo wala jingles ila hilo limekuja kutokana na usemo wake huo.

2. Dudu Baya amekubali ushauri wa kutoa wimbo sasa na kuupa jina la Konko Master kama alivyoshauri na mtangazaji maarufu Fredrick Bundala (skytanzania).

3. Msanii AY ameshauri Dudu Baya kuwahi kusajili msemo huo kabla ya haujaanza kutumika na watu wengine kibiashara hasa kampuni za simu.

"Dudu Baya akitaka kutisha akasajili slogan yake akidelay si mnawajua kampuni zetu za mawasiliano kwa kudandia misemo..PATA OFFER KONKI, Mfikishieni ujumbe wangu," ameeleza AY kupitiamtandao wa Twitter.

Utakumbuka AY na Mwana FA walishinda kesi dhidi ya kampuni ya simu ya Tigo baada ya kubainika ilitumia nyimbo za wasanii hao  kama miito ya wateja wao na kufanya biashara bila idhini ya wasanii hao, Tigo waliamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.