Header Ads

KUNAMBI AWATAKA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI
DODOMA:MKURUGENZI wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi amewataka wafanyabiashara kuwa waaminifu kulipa kodi mbalimbali za serikali ili zisaidie kujenga miundombinu mbalimbali ndani ya jiji la Dodoma pamoja na maboresho ya soko la sabasaba ili liendane na hadhi ya jiji la Dodoma.

Akizungumza na wafanya biashara wa soko la sabasabasa jijini Dodoma Kunambi  amesema kuwa kodi ndio msingi wa maendeo na kuwataka wafanya biashara hao kujitokeza kulipa kodi.

Aidha, kunambi amesema kuwa jiji la Dodoma linapiga hatua kubwa katika maendeleo kwa kupitia kodi ambazo zinalipwa  hivyo jiji linafanya ukarabati mkubwa wa muindombinu ya barabara.

Pia, kunambi ameongeza kuwa kwa sasa jiji la Dodoma watu  wengi wamekuwa wakihamia kwa kasi kubwa , hivyo kama jiji la Dodoma limejipanga kuimarisha masoko ya kila kata ambapo kila kata itakuwa na D center..

Katika hatua nyingine kunambi amesema Mh Rais wa Jamhuriya muungano wa Tanzania  dkt John Pombe Magufuli ameleta fedha  na zimeenza kazi, hivyo wanajenga soko kubwa karibu nchi nzima ambapo soko hilo litakuwa kwaajili ya nafaka na vyakula pamoja na kujenga stendi  kubwa afrika mashariki ambayo itakuwa na maduka makubwa ya kisasa na miradi hiyo inakamilika tarehe 30/9/2019.

Nao baadhi ya wafanya biashara wa soko la sababasa wamesema wanashukuru kwa kuona maendeleo yanayo jitokeza katika jiji la Dodoma  .

Hatahivyo, kunambi ameendelea kuwasisitiza wafanyabiashara hao kuwa mstari wa mbele katika kulipa kodi ya serikali .

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.