Header Ads

MADEREVA WAZEMBE MKOANI NJOMBE KUKIONANJOMBE:Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limeapa kupambana na madereva wazembe ambao wamekuwa wakisababisha ajali za makusudi huku jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani hapa nchini pamoja na vyuo mbali mbali mikoani Vikiendelea Kutoa Elimu Kwa Madereva wa gari za biashara pamoja na gari binafsi Jinsi ya Kuzitambua na Kuzingatia Alama za Barabarani.Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe RENATHA MZINGA amezungumza hilo wakati akifunga Mafunzo ya Siku Tisa Kwa Madereva Mbalimbali Mkoani Njombe Yaliyoandaliwa na Chuo Cha Udereva Cha Future World Driving School Cha Jijini Dar es Salaam huku akiwataka Madereva zaidi ya 200 waliopata mafunzo Wakawe Mabalozi wa Kutokomeza Ajali za Barabarani Kwa Kuhakikisha Ajali Zinapungua zaidi.Ramadhan Sanga,Mahmoud Kankwanzi na Agnes Muugushi ni Baadhi ya Madereva Wapya Waliopatiwa Mafunzo ya Udereva na Alama za Barabarani Ambao Wanasema Sasa Watakuwa Huru Katika Kutumia Barabara Kwa Kuwa Wanafahamu Alama za Barabarani na Kuendesha Kwa Kuzingatia Sheria.


Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Njombe Kelvin Ndimbo Anasema Vyuo Vinavyotoa Elimu ya Udereva Vimekuwa Msaada Mkubwa Kwa Jamii Katika Kukabiliana na Matukio ya Ajali za Barabarani Jambo Ambalo Linapaswa Kuigwa na Watumiaji Wengine wa Vyombo Vya Moto Wasiokuwa na Elimu ya Udereva.Frank Boma ni Mratibu wa Elimu ya Usalama Barabarani Toka Taasisi ya Future World Inayomiliki Chuo Hicho Ambaye Anasema Kuwa Wameendelea Kutoa Elimu ya Usalama Barabarani Katika Mikoa Mbalimbali Hapa Nchini Ukiwemo Mkoa wa Njombe Kwa Lengo Kubwa la Kupunguza Ajali za Barabarani.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.