Header Ads

Mbelgiji Simba afunguka haya kuhusu simba

Mbelgiji Simba Atoa ya Moyoni Kuhusu Yanga
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa kwa sasa hana presha ya kuifuatilia Yanga licha ya kuwa sawa kwa pointi wakiwazidi kwa mabao ya kufunga ambayo yanawaweka nafasi ya pili.

Yanga wana mchezo mmoja mkononi kwa kuwa wamecheza michezo 10 wana mabao 17, Simba wamecheza michezo 11 wana mabao 23, mchezo wa mkononi walionao Yanga unawapa jeuri.

Aussems amesema kuwa pointi sawa na Yanga kumewapunguzia presha hasa kutokana na ushindani uliopo kwenye ligi, hesabu zao kwa sasa ni kuhakikisha wanashinda michezo yao.

"Tupo juu ya Yanga, imeshusha presha kwa kiasi fulani kwa kuwa wao wamekuwa wakifanya kazi yao, sare kwa Ndada sisi ni faida kwetu kwa kuwa tunatakiwa kuangalia mbali ila hilo sio jambo la kutegemea sana," alisema.

Azam wanaongoza ligi kwenye msimamo wakiwa na Pointi 30 baada ya kucheza michezo 12, mabingwa watetezi Simba bado wana imani ya kuleta ushindani kwenye ligi

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.