Header Ads

Michelle Obama afichua jinsi alivyoshika uja uzito wa watoto wake 2


Aliye kuwa mke wa rais wa Marekani Michelle Obama ametoa kumbukumbu ambapo amefichua matatizo aliyopitia katika ndoa yake na uja uzito wa watoto wake wawili.
Katika kitabu hicho, Becoming, Bi Obama amefichua kwamba alitokwa na ujauzito na akalazimika kutumia mbinu ya IVF ambapo mayai ya wapendanao huchanganywa nje na baadaye kuwekwa katika kizazi cha mwanamke kupitia sindano.
Bi Obama aliambia kituo cha ABC Good morning America kwamba alihisi 'amepotea na mpweke' baada ya kupoteza uja uzito miaka 20 iliopita.
Pia alimkosoa rais Donald Trump kwa kuweka usalama wa familia yake hatarini . Bi Obama na mumewe , aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama walilazimika kufanyiwa vikao vya ushauri , na pia alifichua kwamba kwa mara ya kwanza katika kitabu chake chenye kurasa 426 kitakachotolewa siku ya Jumanne.
Kufuatia kuchapishwa kwa kitabu hicho Bi Obama atatembelea miji 10 ikiwemo London.

Alipokuwa mjamzito

Bi Obama , wakili wa zamani na msimamizi wa hospitali aliambia ABC kwamba baada ya kupoteza uja uzito, nilihisi kwamba nimefeli kwasababu sikujua takwimu za kumwagika kwa uja uzito.


''Tunajitenga tukiwa na uchungu'', alisema akiongezea kuwa ''ni muhimu kuzungumza na akina mama wachanga kuhusu ukweli kwamba uja uzito unaweza kukutoka''.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.